HABARI ILIYOTIKISA JIJI-KIMENUKA CCM,MAKADA WAKE WAAPA KUFA NAE MAKONDA,WASEMA MAZITO SOMA HAPA KUJUA
Pichani ni Mwenyekiti wa zamani wa chama hicho Mkoa wa Singida na Kada maarufu wa chama hicho Bwana John Guninita Akizungumza na Waandishi wa Habari Mda huu jijini Dar es Salaam Picha na Exaud Mtei |
KILE
kinachoonekana kwamba hali ya kisiasa ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM imekuwa
sio shwali baada ya Mwenyekiti wa zamani wa chama hicho Mkoa wa Singida na Kada
maarufu wa chama hicho Bwana John Guninita ameibuka na kusema atambuluza mahakamani
–
Katibu wa
vijana na uhamasishaji wa Chama cha
Mapinduzi CCM Paul Makonda mahakamani.Anaripoti KAROLI VINSENT Endelea nayo.
Makonda ambaye sasa ni Mkuu wa Wilaya
wa Manispaa
Hayo yametangazwa na Guninita mda huu
jiji Dar es Salaam wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari Ambapo Mwenyekiti
huyo wa zamani huku akiongozana na Mwanasheria wake ambapo amesema hawezi
kuvumilia unyanyasaji na uonevu anaofanyiwa huku viongozi wa juu wa Chama hicho
wakimfumbia macho.
“leo kijana mdogo kama makonda mtu
ambaye ukimwangalia ni mdogo sana kisiasa hata mimi anaifikii kwa ukongwe wangu
wa siasa leo ananitukana na mamlaka zinamwangalia sasa mimi najiuliza hiki
chama chetu kinauongozi kweli?,mimi siwezi kukubali kama wao viongozi wajuu wanamwachia
kwa maslai nao mimi ila siliogopi nasema naenda mahakamani na nahakikisha
nitamfunga”amesema Guninita.
Guninita ameongeza kuwa madai anayodai
yeye, hayuko peke yake bali yuko na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida bwana Sindai
na amesema kwa sasa haoni haja ya kumsubili na kuwachia aendelee kumtukana
mitaani.
Kuhusu
Kumpiga Jaji warioba.
Gunita
amesema anashangaa sana kijana huyo kumevunjia heshima kutokana na kitendo
chake cha kumpiga jaji warioba na kupewa ukuu wa wilaya.
“Kama chama makini leo kisingempa hata
nafasi ya ukuu wa wilaya maana mtu amempiga Jaji warioba leo anapewa vipi Ukuu
wa wilaya huku akimfanyia vitendo vya kiovu kama kile,harafu anajitetea na kwa
kusema alikuwa mlinzi wa wake hivi mtu hana sifa ya kuwa mlinzi warioba wakatio
ukweli ni huu yeye amempiga warioba na hatufai kabisa kama mnataka muone
nampeleka mahakamani”alisema Guninita.
Alipoulizwa na Waandishi wa Habari
kwanini madai yake asipeleke kwenye Kamati za maadili za chama hicho Guninita
alijipu hawezi kufanya hivyo kutoka na kitendo chake kinaonyesha wazi ni kosa
la jinai.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni