Zinazobamba

HABARI ILIYOTIKISA JIJI--KASHFA KWA ZITTO KABWE,MWIGAMBA NA MSAJILI KUGALAGAZWA MAHAKAMANI SOMA HAPA KUJUA

Pichani ni Mwenyekiti halali wa ACT-Tanzania Kadawi Limbu Akizungumza na waandishi wa habari leo,



NA KAROLI VINSENT
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe ameingia kwenye kashfa nzito,baada ya kudaiwa kumuhonga pesa Msajili wa Vyama vya Kisiasa nchini  ili kuhumjumu Mwenyekiti Halali wa Chama cha ACT-Tanzania Kadawi Limbu ili aondolewe kwenye Nafasi hiyo ili apewe Zitto Kabwe.
      Zitto Kabwe ambaye uanachama wake ndani ya Chama cha Demokrasia Cha Chadema umebakia kwenye makaratasi baada ya  kufukuzwa na uongozi wa Juu wa chadema kwa madai ya kuandaa mipango ya kumuhuju mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe.
       Akifichua Shutuma hizo,Mwenyekiti halali wa Chama cha ACT-Tanzania Kadawi Limbu leo Jijini Dar es Salaam,wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo Limbu akizungumza kwa Uchungu amesema inasikitisha kuona ofisi ya msajili wa vyama  vya siasa nchini ikizorotesha  hususani vya upinzani kwa kuruhusu kuhongwa na Zitto Kabwe.
        “Jamani hili ni jambo la hatari sana mimi leo limbu ni mwenyekiti halali wa ACT nashangaa sana kumuona msajili wa kisiasa anashirikiana na watu ambao mimi nawaona ni majambazi wa siasa nchini wakiongozwa na zitto kabwe kuja kunihujumu mimi ili nitoke kwenye nafasi niliyokuwanayo ,kiukweli sikubali najua wazi kabisia na ushahidi uko wazi kwamba Zitto kabwe amemuhonga Msajili ili mimi nitoke “Amesema limbu.
      Limbu ameongeza kuwa kitendo cha msajili huyo kusema uongozi wake ulikuwa batili kumtimu anayejiita Katibu halali wa ACT-Tanzania Samsoni Mwigamba kwenye nafasi aliyokuwa nayo ni uwongo wa hali ya juu ambao unashusha hazi ya ofisi ya msajili nchini.
     “Kikao tulichotumia kumfukuza  Mwigamba na Profesa Mkumbo kilikuwa halali tena hata kanuni zinaturuhusu wazi kutoa hukumu lakini nashangaa sana ,leo msajili anakuwa upande wa majambazi wa siasa wakiongozwa na zitto kabwe katika kuniondoa mimi lakini najua huyu, msajili ananini na mimi?”amehoji Limbu.
          Aidha,Mwenyekiti huyo wa Zamani wa Chama cha ADC amendelea kumtupia lawama msajili huyo na kusema hatoweza kukubali kuwaachia anaodai ni wahuni wenye nia ya kuubomoa upinzani nchini wa huku wakishirikiana na chama cha mapinduzi CCM.
       “mimi sijawai kuona katika maisha yangu, utoto huu  unaofanywa na  hawa wakina mwigamba na wenzake kwani sababu kubwa ya wao kutaka mimi niondoke ACT ni kukataa mipango ya kukifanya chama hichi cha ACT kuwa ni CCM B na kuubomoa upinzania nchini na kukiweka Chama cha Chadema kuwa Adui wa ACT na mimi nilipokataa wao wakajifanya kugombana na mimi na kuandaa mipango ya kuniondoa ACT”
         Alibainisha kuwa kwa sasa hatoweza kukubali vitendo hivyo anavyofanyiwa na Msajili na Mwigamba  na kusema kwasasa lazima ampeleke msajili huyo mahakamani kwa hujuma hizo.
   “Huyu msajili sio mtu mzuri katika maisha yangu ya siasa na hata nilivyokuwa Kwenye Chama cha ADC alikuwa anifanyia hujuma hizihizi naona leo ameamua kushirikiana na kina Zitto Kabwe,nasema nampelekea mahakamani kwa kitendo chake cha kupokea rushwa naimani nitafanikiwa tu na kufanikiwa huku kutapelekea kuokoa demokrasia nchini”ameendelea kuongeza limbu.
         Kwa upande wake Katibu  mkuu Msadizi wa Chama cha ACT-Tanzania upande wa Bara Leopold Mahona amekitupia lawama  chama cha mapinduzi CCM  kwa kuhusika katika kukifadhili chama cha ACT na kusema yeye hatokubali chama hicho kibakia kwa, anaodai ni wasaliti.
      “Nasema sito kubali kabisa chama chama hichi ambacho mimi Mahona niliyekipigania hadi kupatiwa usajili na mimi ndio niliyemuita mwigamba kwenye chama hichi na kumpa uanachama.lakini nashangaa leo chama chetu tulichokianzisha kwa ajili ya kupambana na chama cha mapinduzi ccm leo ndio kiwe CCM B nasema hatutokuba nipo radhi kufa”amesema Mahona.

Hakuna maoni