Zinazobamba

CCM YAONYESHA UPENDO KWA MAKADA WAKE,YAWATUNUKU KITU MUHIMU SOMA HAPA KUJUA

Katibu wa CCM mkoa wa Tabora Bi.Jannat Kayanda akimkabidhi cheti mmoja kati ya makada wa chama hicho Bw.Emmanuel Mwakasaka waliokisaidia kupata ushindi wakati wa uchaguzi wa Serikali za mitaa,vijiji na vitongoji wilaya ya Tabora mjini ambapo CCM ilipata ushundi mkubwa dhidi ya vyama vya upinzani.
Katibu wa CCM mkoa wa Tabora Bi.Jannat Kayanda akizungumza katika maadhimisho ya 38 ya kuzaliwa kwa CCM ambapo aliwataka wananchi kuendelea kukiamini chama hicho kwakuwa kimewaletea maendeleo ikiwa ni pamoja na kudumisha amani na utulivu wa Taifa.
Hawa ni makada mahili wa CCM mkoa wa Tabora("MAJEMBE YA CCM TABORA")ambao wametambulika michango yao katika kukisaidia chama kwa hali na mali na kuhakikisha chama kinaendelea kujenga heshima yake katika kuwaongoza wananchi.
Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Tabora mjini ambaye ni kada wa chama hicho  Bw.Emmanuel  Mwakasaka akionesha heshima ya utii mbele ya viongozi baada ya kupokea cheti cha kumpongeza na kutambua mchango wake katika kukisaidia chama kupata ushindi uchaguzi wa Serikali za mitaa,vijiji na vitongoji wa mwaka 2014 ambapo CCM iliibuka mshindi dhidi ya vyama vya upinzani

Hakuna maoni