WEZI WAZIDI KULITESA SHIRIKA LA TANESCO,WAIBA WAYA WENYE THAMANI YA MAMILIONI-SOMA HAPA KUJUA
Kituo kinachomilikiwa na shirika la Umeme nchini Tanesco picha na maktaba picha kamili itakujia |
NA KAROLI
VINSENT
WATU
wasiojulikana wamekivamia kituo cha upozaji na usambazaji wa umeme nchini TANESCO kilichopo Uwanja wa ndege Jijini Dar es Salaam na
kuiba waya wenye Thamani ya Milioni 150 za kitanzania na kutokomea kusiko
julikana
Na kulifanya Shirika la Umeme
nchini kukwama kuwasha Jenereta za kituo hicho ambacho walitarajia kuwanya
mwezi marchi mwaka huu.
Akithibitisha kutokea kwa wizi huo
Mda huu Jijini Dar es Salaam Meneja wa ugawaji na usambazaji wa Umeme wa shirika hilo bwana Emmanueli Maniraboma Wakati alipotembelewa na vyombo mbalimbali vya Habari,ambapo alisema wizi huo wa waya
umekwamisha mipango ya kuwasha mitambo mbalimbali ya umeme kituoni hapo.
“Kutokana na
wizi huu tumekwama kufanya mambo mengi yenye maendeleo katika kituo
hiki,kwani tulitarajia kuwasha mitambo hii ili watumiaji wa umeme watumia vizuri na kutokana wizi huu,sasa tumekwama kabisa”alisema Bwana Maniraboma.
Bwana Maniraboma
aliongeza kuwa waya hizo zilizoibia hazipatikani nchini na mpaka kuzileta nchini ilitumia zaidi ya milioni 150
za kitanzania kwa kutumia usafiri wa meli na wakitumia usafiri wa ndege gharama zitaongezeka na kufikia fedha za kitanzania zaidi ya milioni
200.ambapo uagizaji wake utachukua zaidi ya miezi mitatu.
Aidha,bwana
Maniraboma alisema kutokana na wizi huo shirika limechukua hatua ikiwemo
kufanyia uchunguzi juu ya hujuma wizi huo na ikibainika hatua kali za kisheria
zichukuliwe kwa walinzi wanaorinda kituo hicho.
Kwa upande wake
Afisa Mwandamizi wa sheria na Uchunguzi wa Shirika la Umeme TANESCO lenin
Kiabya alisema kwa sasa wako kwenye uchunguzi ikiwemo kwa walinzi wanaorinda
kituoni hapo na ikibainika kama wao walizembea mpaka wizi huo kutokea
watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni