VIJANA WENGI NI WALEVI WA VIROBA,WASEMA TAMWA SOMA HAPA KUJUA
Pichani ni Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari nchi TAMWA BI Varelia Msoka akifafanua jambo picha na Maktaba |
NA KAROLI
VINSENT
CHAMA cha
Waandishi wa Habari wanawake TAMWA kimesema vijana wengi katika Jijini la Dar es Salaam
hususani Wilaya ya Kinondoni ni Walevi kupita kiasi na kupelekea kuongezeka
unyanyasaji wa kijinsia katika maeneo hayo .
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam
na Mtendaji wa chama cha Waandishi Wanahabari
nchini TAMWA Bi Varelia Msoka wakati wa semina kwa waandishi wa habari
kuhusu kuripoti ya habari za watu waliokumbana na vitendo vya unyanyasaji wa
kijisinsia,ambapo pamoja na mambo mengine alisema kwa sasa hali ya vijana-,
Kujiingiza
katika vitendo vya matumizi ya pombe vimeongezeka kwa kiasi kikubwa na kutishia
maendeleo kwa vijana.
“Tulifanya utafiti katika
wilaya ya kinondoni kwenye baadhi ya kata tukabaini vitendo vya utumizi wa
pombe hususani viroba vimeongeza kwa kiasi kikubwa na kwani kila duka vinywaji
hivyo vya viroba vinauzwa huku watumiaji wengi wakiwa vijana tena wenye elimu
wanatumia vilevi hivyo”
Bi Msoka aliongeza kuwa licha ya wilaya
ya kinondoni kuwa na vyuo vikuu vingi ambavyo ni Chuo kikuu cha Mlimani,Chuo
kikuu huria na chuo kikuu cha Tumaini lakini bado jamii ya wasomi imeshindwa
hata kutoa elimu kwa vijana kuacha utumiaji wa pombe.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Tamwa, Gladness Munuo aliitaka serikali za mtaa pamoja na za vijiji
kuona haja ya kutoa elimu kwa vijana na kutoa matamko kuishinikiza serikali kuu
ili kupambana na vitendo vya unywaji pombe kwa vijana hasa kipindi cha kazi.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni