HABARI KUBWA-VIDAGAA WENGINE WA ESCROW WAPANDISHWA MAHAKAMANI,RUGIMALIRA AZIDI KUWAPONZA SOMA KUJUA
NA KAROLI
VINSENT
SIKU moja
kupita baada ya Taasisi ya kupambana na kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kuwapandisha
washtakiwa wawili kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam kwa
tuhuma za kupokea Rushwa kutoka kwa Mkurugenzi wa VIP Engineering bwana James
Rugimalira ambapo pesa hizo ni za Akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa Benki Kuu (BOT).
Hatimaye tena leo Taasisi hiyo ya kupambana na Rushwa (TAKUKURU)
imewapandisha watendaji wengine wa
serikali kwa kosa ya kupokea Rushwa zenye Thamani ya zaidi ya Bilioni 2.6 za
kitanzania kutoka kwa mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering bwana James Rugimalira
ambazo pia ni pesa za Akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa BOT.
Wakisomewa Mashtaka yao kwa nyakati
Tofauti kwenye Mahakama ya hakimu mkazi kisutu watuhumiwa hao Mwanasheria
mwandamizi wa Shirika la Umeme nchini TANESCO Steven Urassa akisomewa shtaka lake Mwanasheri wa TAKUKURU Bwana Leonard Swai mbele ya hakimu Devota Kisila ambao ilidaiwa mtuhiwa alipokea
Rushwa kutoka kwa Bwana James Rugimalira kupitia Akaunti ya Bank ya Mkombozi
milioni 194 huku akijua anafanya kosa.
Mwengine ni Kyabukoba leonald Mutigwa
ambaye naye ni Meneja wa Kodi kutoka
Mamlaka ya kodi nchini (TRA) ambapo pia alisomewa shtaka na Mwanasheria
wa TAKUKURU bwana Leonald Urassa anadaiwa kupokea Rushwa ya milioni 191 kutoka
kwa mkurugenzi wa VIP Engineering Bwana James Rugimalira kupita Akaunt ya Banki
ya Mkombozi.
Vilevile mwengine pia ni Julius Rutta
mkurugenzi wa Benki Kuu nchini (BOT) naye alifikishwa makamani hapo na kusomewa
shtaka lake na Bwana Leonald Swai mbele
ya Hakimu Janeth Kalugenda ambapo anatuhiwa na TAKUKURU kupokea Rushwa ya Milioni 382 pamoja na
Bilioni 1 kutoka kwa Mkurugenzi wa VIP Engineering bwana James Rugimalira huku akijua ni kosa.
Kati ya
watuhuiwa watatu Mtuhumiwa mmoja tu Bwana Steven Urassa ndio aliyekizi vigezo
vya Dhamana na sasa yuko nje lakini wengine wameendelea kusota Rumande.
ENDELEA
KUFUATILIA MTANDAO HUU UTAPATA ZAIDI KWA UREFU
Hakuna maoni
Chapisha Maoni