HABARI KUBWA LEO-UKAWA WAMSUSIA KIKWETE KATIBA YAKE-WAGOMA KWA KILA KITU,SOMA HAPA KUJUA
Pichani ni Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahimu Lipumba picha na Maktaba |
UMOJA wa
Kutetea katiba ya Wananchi UKAWA umesema
utasusia zoezi la upigaji wa kura wa Katiba
iliyopendekezwa na Bunge Maalum la katiba inayotarajiwa kupigwa mwezi wa nne
mwaka huu kwa Madai Rais Jakaya Kikwete
amekiuka makubaliano na Vyama vya siasa waliokubaliana mwaka jana mjini Dodoma .Na KAROLI VINSENT anaripoti. Endelea nayo.
Azimio hilo limetangazwa leo Jijini
Dar Es Salaam na Mwenyekiti mwenza
wa Umoja wa vyama Vikuu vya Upinzani vinavyounda Umoja wa kutetea Katiba ya
Wananchi UKAWA Freeman Mbowe, wakati wa mkutano na Waandishi wa habari ambapo
amesema Umoja huo hauwezi kuwepo katika mipango ya kuingamizi nchi wakati wa kupitisha
katiba isiyokuwa na chembe yeyote ya kumsaidia mtanzania.
“Tunasema
kwa pamoja hatutoshiriki katika katika kura za wa kupitisha katiba ya chama cha
Mapinduzi,katiba iliyotengenezwa bila ya kuwa na maridhiano ya Kisiasa,maana
Rais Kikwete ameamua kwa makusudi kabisa kutusaliti sisi viongozi wenzake wa
kisiasa,tulikubaliana kwamba Bunge lile lisitishwe kutokana na kutoweza
kupatikana kwa katiba mpya lakini alivyotoka pale akatusaliti na kuendelea na
Bunge lile lilotafuna pesa za wananchi walalahoi”alisema mbowe.
Mbowe aliongeza kuwa katika makubaliano
hayo walifikia maazimio ya kufanyia mabadiliko katiba iliyopo ya mwaka 1977
katika vipengele mbalimbali ikiwemo kipengele cha kuwepo tume huru ya uchaguzi
lakini Rais Kikwete akawageuka dakika za mwisho.
Mbowe ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Hai
alizidi kusema kwa uchangu kwamba Umoja huo umebaini rafu mbalimbali
wananazozifanya Chama cha mapinduzi ili katiba iliyopendekezwa iwe katiba
harala kwa kuwasafirisha watu kutoka Mkoa wa dare s Salaam hadi Visiwani Unguja
na pemba ili wakati wa kupiga kura ya kupitisha katika Iliopendekwa na bunge
waipigie kura ya Ndio ambapo mbowe anasema wao hawatakubali.
vyama hivvyo
Vinavounda UKAWA ni CUF,Chadema,NCCR
mageuzi na NLD
Kwa
upande wake mwenyekiti wa chama cha NLD Dk. Emmanuel Makaidi amesema chama chake kitazunguka nchi nzima
kuhamisha wananchi kutopigia kura katiba pendekezwa kwa Madai Katiba hiyo
inamapungufu kibao na itazidi kuwaweka katika mazingira magumu yenye kujaa
umasikini.
Naye Mwenyekiti wa chama cha NCCR
Mageuzi James Mbatia alisema anashangaa
kitendo cha Rais Kikwete kuwageuka na kuyatupia mbali makubaliano yao waliosema mchakato usitishwe
mpaka baada ya uchaguzi mkuu na kufanyia marekebisho ya Katiba iliyopo na
kusema kitendo hicho kinaonyesha kiongozi huyo alivyokuwa kigeugeu na umoja
huo hautokubali.
Vilevile Mwenyekiti wa Chama cha
Wananchi CUF Profesa Ibrahimu Lipumba alisema Katiba wanayoitaka kuipitisha
kinguvu haina mshiko kwa watanzania na imekaa kwa ajili ya kuwanafaisha
watawala walioko madarakani,na akasema chama chake hakitokubali kuwepo katika
dhambi ya kuwahujumu wa Tanzania na wao
watasusia mchakato huo.
ENDELEA KUFUATILIA MTANDAO HUU HABARI KAMILI INAKUJIA
Hakuna maoni
Chapisha Maoni