DAWA HIZI NI HATARI KWA AFYA YAKO,TFDA YASEMA WANANCHI WAWE MAKINI SOMA HAPA KUJUA
Pichani ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini TFDA Bwana Hiiti Sillo akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar Es Salaam |
NA KAROLI
VINSENT
MAMLAKA ya
Chakula na Dawa nchini (TFDA) imezifutia Usajili na kuzuia Uingizaji Dawa tano za Binadamu kutokana na kuwepo makosa
mbalimbali.
Hayo yametangazwa leo jijini Dar es
Salaam na Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya
Chakula na Dawa nchini (TFDA)Bwana Hiiti Sillo Wakati wa Mkutano na Waandishi
wa Habari ambapo alisema Mamlaka hiyo katika kupitia mifumo ya ufuatiliaji wa usalama na ubora wa dawa nchini wamebaini
uwepo wa dawa duni kwenye soko zenye madhara na zisizofaa kwa matumizi ya
Binadamu.
Ambapo katika kufuatilia huko,Mamlaka
hiyo imefikita hatua ya kufuta wa usajili wa aina tano za dawa za binadamu ,ambazo
ni Dawa ya kutibu “Fungus” ya vidonge na kapsuli aina ya ketocanazole ambayo
mamlaka hiyo imesema sababu ya kuzuia kwake ni kutokana na kubaini dawa hiyo
inasababisha madhara hatarishi katika Ini kwa watumiaji.
Na nyingine ni dawa ya kutibu malaria ya maji na
vidonge aina ya Amodiaquine nayo pia Mamlaka hiyo imesema sababu ya kufutia usajili
na kuzuia kuingia nchini kutokana na mabadiliko ya mwongozo wa kisera wa kupima
na kutibu malaria wa mwaka 2013 wizara ya Afya na Ustawi wa jamii ambapo
mabadiliko hayo yamebaini Amodiaquine ikitumika peke yake inaleta usagugu wa
vimelea vya malaria.
Mkurugenzi huyo aliitaja dawa nyingine ambayo ni hatari kwa binadamu ni Dawa ya kutibu mafua na kikohozi za Maji,Vidonge na
kapsuli zenye kiambato hai aina ya Phenylpropanol amine ambacho anasema
kinaleta madhara hatarishi kwa binadamu kama vile kiharusi (Hemorrhagic sroke).
Mbali na hizo Dawa zengine ni Dawa
ya kuua bacteria ya Sindano aina ya Chloramphenic ol Sodiam Succinate
inayotengenezwa nchini India pamoja na dawa ya kuua Bakteria ya Maji na kapsuli
aina ya Cloxacillin ambazo zote kwa pamoja bwana Fimbo alizitaja kwamba zina
madhara kwa watumiaji ikiwemo kushindwa kupumua na kupoteza Fahamu.
Katika Hatua Nyingine mamlaka hiyo
imebadili na kudhibiti aina nne ya dawa mbalimbali.
Dawa hizo ni Dawa ya kutibu
imebadilika matumizi yake,maralia ya vidonge yenye mchanganyiko wa Sulphadoxine
na pyrimethamine na dawa aina ya Kanamycin Amikacin na Levofloxian.
Aidha Bwana Sillo aliwataka wamiliki wa
maduka ya Dawa,pamoja wananchi kuzingatia taarifa zinazotoka kwenye Mamlaka
hiyo ili wasikumbane na matatizo na akazitaka Hospitali mbalimbali nchini
pamoja maduka ya dawa kuaacha kuuza dawa hizo mala moja.
Maoni 1
ok. got the info.
Chapisha Maoni