FUKUZA NI NIKUFUKUZE NDANI YA CHAMA CHA ACT,LIMBU ASEMA HATUKUBALI KUWAACHIA WAHUNI CHAMA SOMA HAPA KUJUA
Pichani ni Anayejiita katibu Mkuu wa ACT-Tanzania, Samson Mwigamba |
LUCAS Limbu, mwenyekiti wa Chama cha Alliance for change and
Transparence (ACT), ameendelea kung’ang’aniza kuwa Samson Mwigamba na Prof.
Kitila Mkumbo, siyo wanachama wa chama hicho.Sarafina Lidwino, anaandika.
Limbu, mwenyekiti wa chama hicho ngazi
ya taifa na ambaye anatambulika na Sheria Na. 5 ya vyama vya siasa anasema,
Prof. Kitila na Mwigamba, tayari wameshafukuzwa na hakuna mwenye ubavu wa
kuwarejesha ACT-Tanzania.
Mwenyekiti alikuwa akizungumzia
kinachoitwa “uchaguzi unaoendelea ndani ya chama” chake. Alisema ndani ya ACT
kwa sasa, hakujawa na uchaguzi.
“Nikiwa mwenyekiti halali wa chama hiki,
naomba ieleweke wazi kwamba, bado hatujatangaza taratibu za uchaguzi. Uchaguzi
unaofanyika katika ngazi za vijiji na kata, siyo wa ACT- Tanzania. Huo ni
uchaguzi wa chama cha Mwigamba na Prof. Kitila,” ameeleza.
Amesema, wanaotisha uchaguzi – Prof.
Kitila na Mwigamba – siyo viongozi wala wanachama wa chama chake na hivyo
hawana mamlaka ya kuitisha uchaguzi.
Alikuwa akizungumza na
waandishi wa habari, katika ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo), jijini Dar es
Salaam.
Prof. Kitila na Mwigamba wamefukuza
uanachama kwa makosa ya kuanzisha chama ndani ya chama.
Chama cha ACT kinachoongozwa
kinyemela na Zitto Kabwe, mbunge wa Kigoma Kaskazini; Mwigamba na Prof. Kitila,
ni mawakala wake.
Limbu amewataka wanachama wa
ACT wawe watulivu, wakati ofisi ya msajili wa vyama ikiendelea kupitia nyaraka
zao za mabadiliko ya uongozi
Hakuna maoni
Chapisha Maoni