YAMEFICHUKA-FAMILIA YA KIKWETE YAFAIDIKA NA ESCROW,ASEMA MARANDO,ASEMA MAZITO SOMA HAPA KUJUA
pichani ni Rais Kikwete, |
RAIS Jakaya Kikwete anapaswa kuwajibika binafsi katika kashfa ya
ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Tegeta Escrow. Saed Kubenea
anaandika…(endelea)
Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mabere Marando amesema, Rais Kikwete,
ndiye aliyeruhusu kiasi cha Sh. 321 bilioni kuchotwa katika mazingira
yaliyosheheni udanganyifu.
“Fedha zile zimechukuliwa kwa maelekezo
ya Rais Kikwete ili kumuwezesha chama chake kufanikishe kampeni za uchaguzi
mkuu wa mwaka huu,” ameeleza Marando.
Hata hivyo, Marando anasema, “Tumeambiwa
na watu waliokaribu na chama hicho, kuwa ni sehemu ndogo sana ya fedha
iliyoibwa zilizofikishwa CCM. Nyingi ya fedha hizo zimechukuliwa na familia ya
rais mwenyewe.”
Taarifa zinasema, familia ya
Rais Kikwete imepata zaidi ya Sh. 9 bilioni, kutoka katika mgawo wa fedha
zilizohifadhiwa katika akaunti ya Escrow.
“Kikwete anajua kila kitu. Yule
singasinga – Harbinder Singh Sethi – alitokea Ikulu. Mpango wa uchotaji wa
fedha za umma ulipangwa Ikulu na ulitekelezwa kwa maelekezo ya rais,” ameeleza.
Taarifa zinasema, anayejiita na
kuitwa na serikali kuwa ni “mmiliki mpya wa IPTL/PAP,” Harbinder Singh Sethi,
alichotewa fedha hizo baada ya kufikishwa Ikulu na baadaye akakutanishwa na
gavana wa BoT, Prof. Benno Ndullu; na kutoka hapo alikwenda kukwapua mabilioni
hayo ya shilingi hata bila kumfahamisha James Rugemalira – mbia mwenzake.
Sakata la ukwapuaji wa fedha katika
akaunti ya Escrow ndilo lililomtupa nje ya ofisi, aliyekuwa waziri wa nishati,
Prof. Sospeter Muhongo.
Taarifa zinasema, Prof. Muhongo, ni
miongoni mwa wanaotajwa kunufaika na fedha za Escrow zilizopitia benki ya
Stanbic. Mwingine ambaye jina lake lilitajwa bungeni na mmoja wa wabunge wa
upinzani, ni Albert Marwa.
Marando anasema, “Pamoja na kujiuzulu
kwa Prof. Muhongo, bado haitoshi bila kuhojiwa au kuwajibishwa kwa gavana
Ndullu, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, Katibu Mkuu wizara ya Fedha, Dk.
Servacius Likwalile na maofisa wa ikulu na hata rais mwenyewe ambaye ndiye
aliyeruhusu fedha hizo kutolewa.”
Akiongea kwa kujiamini, Marando
anasema, “Wizi huu ulianzia Ikulu na umefanyika kwa baraka za Ikulu na mbele ya
macho ya rais. Umewashirikisha baadhi ya maofisa wake na hata familia yake.”
Dk. Likwalile ndiye aliyewasilisha
kwa gavana wa BoT kwa ajili ya utekelezaji, maagizo ya Rais Kikwete kuwa fedha
katika akaunti ya Escrow zilipwe kwa PAP.
Alikuwa akirejea maagizo kutoka kwa Rais
Kikwete kwa kunukuu barua ya tarehe 13 Novemba 2013, ambayo ilisainiwa na
Katibu wa Rais, Bw. Prosper Mbena.
Chanzo ni
gazeti la mwanahalisi online
Hakuna maoni
Chapisha Maoni