Zinazobamba

WLAC YAZINDUA REPOTI YAKE KUHUSU WATOTO WALIO MAGEREZANI,

VICTORIA MGONELA ambaye ni mtaalam wa ulinzi na usalama wa mtoto UNICEF ambao wao ndio wadau wakubwa wa WLAC waliofanikisha kupatikana kwa report hiyo akizungumza katika hafla hiyo
  Kaimu mkurugenzi wa WLAC BI GRACE DAFA amesema kuwa hapo awali walikuwa hawatoi msaada wa kisheria kwa makosa yanayowahusu watoto lakini ilipofika mwaka 2000 kwa kushirikiana na shirika la umojawa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF wakaanza kutoa msaada huo wa kisheria kwa kutumia sharia ya mwaka 2009 ya watoto ambayo ilitaka watoto wenye makosa wahukumiwe kama watoto na sio watu wazima na ndipo shirika hilo lilianza rasmi kuwatetea watoto.
 

Mwanasheria mkuu wa WLAC ROBERT CHUWA ambaye ndiye moja ya watuwalioandaa report Akizungumza jambo mbele ya wadau kuhusu repoti hiyo iliyozinduliwa mapema hii leo
Chama cha wanawake wanasheria Tanzania WLAC kimeibuka na repoti ambayo inaonyesha kuwa Wabakaji wengi wa watoto wamekuwa wakidaganya umri na hivyo kuwapelekea sheria kushindwa kuwahukumu kama watu wazima,

Hayo yamebainika leo wakati wakizindua report yao ya hali ya watoto waliopo katika magereza kwa makosa mbalimbali ya jinai report ambayo inaonyesha bado kuna changamoto mbalimbali zinazowakuta watoto wanaotumikia adhabu mbalimbali katika magereza huku wadau wakiombwa kuwatafitia ufumbuzi watoto hao kwani bado ni msaada kwa taifa.
 Wlac imestushwa na wimbi la watu wazima ambao wamekuwa wakidanganya umri ili kuweza kukwepa hukum na hivyo kupelekea watoto walioathirika kujisikia vibaya,
Unakuta mtu mzima wa miaka 26,27 wanadanganya umri wakijua fika kudanganya kwao umri kunawasaidia kujiepusha na adhabu kali ya mahakama


Akisoma mambo kadhaa yanayopatikana katika report hiyo mwanasheria mkuuwa WLAC ROBERT CHUWA amesema kuwa moja ya changamoto kubwainayowakumbawatoto wanaotumikia adhabu katika magereza yetu ni pamoja na kutokuwa nauelewa wa kutosha kuhusu makosa waliyofanya pamoja na kukosa watu wakuwapa elimu hiyo kwa muda muafaka.

Aidha amesema kuwa chanagamito nyingine iliyopo katika mahakama zetu pamoja na polisi watoto kudanganya umri wao pindi wanapokutwa na makosa kwa lengo la kuepuka adhabu za watu wazima na kudanganya kuwa wana umri chini ya miaka 18.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa katibu mkuu wizara ya katiba nasharia mh MAIMUNA TARISHI pamoja na kuwapongeza WLAC pamoja na wadauwengine kwa kutoa msaada wa kisheria kwa watoto waliopo magerezaniamesema kuwa serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wanaendelea
kuwasaidia watoto hao kwa hali na mali kwani wanatambua fika kuwa watotohao wanahitaji msaada wa kisheria ili kubadilika na kuwa katika hali nzur
 Awali akizungumza kaim mkurugenzi wa WLAC BI GRACE DAFA amesema kuwahapo awali walikuwa hawatoi msaada wa kisheria kwa makosa yanayowahusuwatoto lakini ilipofika mwaka 2000 kwa kushirikiana na shirika la umojawa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF wakaanza kutoa msaada huo wa kisheria kwa kutumia sharia ya mwaka 2009 ya watoto ambayo ilitaka watoto wenye makosa wahukumiwe kama watoto na sio watu wazima na ndiposhirika hilo lilianza rasmi kuwatetea watoto.
 
Shirika la WLAC lilianza rasmi kufanya kazi zake mnamo mwaka 1989 nchini Tanzania na hadi sasa limekuwa na mafanikio makubwa kwa kutoa msaada wa kisheria katika Nyanja mbalimbali
 

Hakuna maoni