VIJANA MPO? TANGAZO MUHIMU KUTOKA JKT HILI HAPA
MAFUNZO YA VIJANA WA JKT (KUJITOLEA).
TANGAZO LA MKUU WA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA VIJANA WOTE WANAOTAKA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA UTARATIBU WA KUJITOLEA MWAKA 2015.
UTARATIBU UTAKUWA KAMA IFUATAVYO:
BARUA ZA MAELEKEZO ZITATUMWA MIKOANI FEBRUARI 2015, MCHAKATO WA KUCHAGUA VIJANA WILAYANI NA MIKOANI (MACHI HADI APRILI 2015), TIMU ZA USAILI TOKA MAKAO MAKUU YA JKT ZITAKUWA MIKOANI MEI 2015 NA VIJANA WALIOCHAGULIWA KURIPOTI VIKOSINI JUNI 2015.
LINATOLEWA ANGALIZO KWA VIJANA, WAZAZI/WALEZI KUEPUKA KUDANGANYWA NA MATAPELI WANAOJIHUSISHA NA UUZAJI WA FOMU BANDIA ZA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA.
FOMU ZINAZOTOLEWA SASA NI BATILI. JESHI LA KUJENGA TAIFA HALITATAMBUA USAILI WOWOTE UTAKAOFANYIKA KINYUME NA UTARATIBU ULIOAINISHWA.
TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA MAKAO MAKUU
Hakuna maoni
Chapisha Maoni