SAKATA LA ESCROW.... HAYA NDIYO MAAMUZI YA SERIKALI YA KIKWETE
Rais
Jakaya Kikwete ametengua nafasi ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kupitia hotuba aliyotoa kuzungumzia
kashfa ya upotevu wa fedha kutoka akaunti ya Tegeta Escrow.
Hatua
hiyo imechukuliwa na Rais Kikwete mbele ya wazee wa Dar Es Salaam
aliokuwa akiongea nao na matangazo kurushwa moja kwa moja kupitia
televisheni ya taifa na vyombo vingine.
Uchunguzi uliofanywa na
kamati ya hesabu za umma ya Tanzania (PAC), ilidai kuwa Profesa
Tibaijuka ni mmoja wa watu walionufaika kinyume cha sheria kwa kupata
fedha zilizotoka katika akauti hiyo iliyofunguliwa kutunza fedha
kusubiri ufumbuzi wa mgogoro wa kibiashara kati ya kampuni ya kusambaza
umeme TANESCO na kampuni binafsi ya kuzalisha umeme ya IPTL.
Siku
chache zilizopita Profesa Tibaijuja aliitisha mkutano na waandishi wa
habari jijini Dar Es Salaam kubainisha kuwa hakuwa akikusudia kujiuzulu
kutokana na tuhuma zilizokuwa zikimkabili.
Hata hivyo Rais Kikwete
hakutangaza kuwachukulia hatua watumishi wengine waliodaiwa kuhusika na
tuhuma hiyo kwa maelezo kuwa uchunguzi zaidi unatakiwa kwa kila
mtuhumiwa.
Kumekuwa na ubishi mkubwa kujadili endapo fedha ambazo
ni mabilioni zilizochukuliwa zilikuwa za umma au la. Na hata Rais
Kikwete amesema maelezo aliyopewa na wataalam yanaonyesha hazikuwa mali
ya TANESCO.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni