MBUNGE NASSARI APONEA CHUPUCHUPU,NI KUTOKANA NA KESI INAYOMKABILI SOMA HAPA KUJUA
Na Woinde shizza, Arusha
Hakimu David Mwita wa Mahakama ya mwanzo ya Maji ya Chai mkoani Arusha ameahirisha hadi Desemba 24, 2014 kesi inayomkabili Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Mh. Joshua Nassari (pichani), kwa tuhuma za kuharibu mali ya umma yenye dhamani ya shilingi laki mbili, pamoja na kumteka mtu na kumtishia kwa bunduki tukio ambalo anatuhumiwa kufanya Desemba 15, mwaka huu
Mahakama hiyo imemuachia Mbunge huyo baada ya kutimiza masharti ya dhamana, ikiwa ni wadhamini watatu ambao wana mali zisizohamishika zenye thamani ya shilingi milioni moja na nusu kila mmoja.
Akiongea mara baada ya kuairisha kesi hiyo wakili wa mbunge huyo wa Arumeru mashariki Bw. James Ole Milya alisema kuwa amesikitishwa sana na tukio la mahakama hiyo kumpa mashariti makubwa mteja wake kwani kesi yake ilikuwa haihitaji mashariti makubwa hivyo .
Aidha alisema kuwa mbali na kupewa mashariti hayo angependa kesi hiyo ipelekwe katika mahakama ya wilaya ili yeye kama wakili wa mbunge huyo aweze kumtetea kwani katika mahakama ya mwanzo hairuhusu kuweka wakili.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni