KAMANDA KOVA AZIDI KUJIDHATITI KULEKEA SIKUKU ZA XMASS NA MWAKA,AONGEZA POLISI WAPYA. SOMA HAPA
Na Karoli
Vinsent
KAMISHNA wa Polisi
Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam amewapokea askari waliomaliza mafunzo ya
uongozi mdogo wa Jeshi hilo la Polisi katika vyuo vya Polisi vya Moshi na
Zanzibar ambao ni utaratibu wa kawaida na kuwaasa mambo mbalimbali.
Akiwapokewa Askari hao Juzi Kamishna wa
Kanda Maalum ya Polisi Suleiman Kova na kushuhudiwa na Viongozi mbalimbali wa
Jeshi la Polisi pamoja na Waandishi wa Habari ambapo amewataka Amewataka
kutumia ujuzi na maarifa walivyopata katika mafunzo yao ili kuondoa kero za
uhalifu katika jiji la Dar es Salaam.
“Matukio ambayo ni kero
katika jiji la Dar es Salaam ni pamoja na matumizi ya Dawa za kulevya, ujambazi
wa kutumia silaha, na kero nyingine, madanguro, grocery katikati ya barabara,
na muziki unaopigwa kiholela katika makazi ya watu”. Alisema Kamishna Kova.
Kamishna Kova alizidi kuwataka
Askari hao washirikiane na askari wenzao katika oparesheni inayoendelea jijini
Dar es Salaam kuanzia mwezi Oktoba hadi Desemba ili kuthibiti vitendo vya
uhalifu ambavyo kwa kawaida hujitokeza kwa wingi katika kipindi hichi.
Vilevile Kamishana huyo alizidi kuwahasa tena wahitimu hao kutakiwa kusimamia na kudumisha
nidhamu katika Jeshi la Polisi ili kuwafanya wananchi wapate huduma nzuri
pamoja na kuleta taswira nzuri ya Jeshi
la Polisi.
Maaskara wapya wakiwa Tayari kwa kazi Jijini Dar es Salaa picha na Polisi |
Aidha,Kova aliitaka jamii kushirikiana
na Askari hao wapya katika kulinda Amani katika maeneo mbalimbali ya Jijini
hapa hususani katika kipindi hiki cha Sikuku za Mwisho wa Mwaka.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni