HOTNEWS-MHARIRI WA GAZETI LA TANZANIA DAIMA NUSURA WAPIGANE NA NYAMBUI,SOMA HAPA KUJUA
Pichani ni Katibu Mkuu wa Mchezo wa Riadha nchini Suleiman Nyambu akifafanua Jambo kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari jana Picha na Suleiman Magari |
Na Karoli
Vinsent
KATIKA hali
isiyokuwa ya Kawaida Kaimu mhariri wa Gazeti la Tanzania Daima Tullo Chambo na
pia Mjumbe wa Taifa wa Riadha (RT) nusura wapigane na Katibu mkuu wa Riadha
Taifa (RT) Suleiman
Nyambui kutokana na kupenyezwa jina la
kiongozi atakayesimamia mashindano ya Uhuru Marathoni ambapo Mhariri huyo akuridhika
Hayo
yalitokea jana wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari uliitishwa na Waandaaji
wa Mashindano Uhuru marathoni
kuzungumzia mashindano hayo yanafanyika wiki ijayo,ambapo Katibu wa Riadha
Taifa Suleiman Nyambui alipopewa nafasi kiongozi wa Riadha Taifa
kuzungumzia mashindano hayo ndipo akawataja
viongozi watano watakaosimamia-
Shughuli nzima,ambapo baada ya kutajwa
majina hayo ndipo Mwandishi huyo Mwandamizi na pia Mhariri wa Gazeti la Tanzania
Daima akanyosha mkono ili kupewa nafasi ambapo alipopewa Nafasi alipinga na
kusema majina ya viongozi hao kusimamia Mashindano hayo hayajathibitishwa na
viongozi pamoja na Wajumbe wa Taifa wa mchezo wa Riadha nchini.
Baada ya Mhariri Tullo kusema hivyo huku
Nyambui akiwa amechukizwa na kitendo cha mhariri huyo kusema ukweli,ikamfanya
Mratibu wa Mashindano hayo Innocent
Melleck kumtaka Tullo chambo kuacha kumzungumzia suala hilo kwakuwa Dhumuzi la
kuitisha Mkutano na Waandishi wa Habari halikuwa suala hilo na kuwataka waende
wakazungumzia kwenye mikutano yao.
Licha Bwana Melleck kusema hivyo baada ya
Mkutano huo Kumalizika na Waandishi wa Habari bado Majibizano yaliendelea huku
sasa ikiwa nusura wapigane baada ya Tullo Chambo kumtaka Katibu Nyambui asema
ukweli kwa watanzania kwani amewateua watu anawajua yeye kusimamia mashindano
hayo huku wengine sio viongozi wa Mchezo wa Riadha nchini,
Ambapo baada ya kusema hivyo Katibu huyo
akataka kumfuata Tullo ili kupigana nae mambo hayakuwa hivyo baada ya Jitihada
zilizofanya na Waandishi wa Habari ziliweza kumzuia Katibu huyo kutaka kufanya
Jambo hilo la Ajabu.
Ndipo Jitihada hizo zilizaa matunda na
baada ya watu hao wawili kutuliza Ghaziba walizokuwa nazo.
Huku wawili hao wakiwa wametuliza Hasira
zao,Mwandishi wa Mtandao huu alipokuwepo Mkutanoni hapo,alipomfuata Mratibu wa
Mashindano hayo ya Uhuru Marathoni kutaka kujua kulikoni anamruhusu kiongozi
huyo kufanya Mambo ambayo hayana Utaratibu alisema.
“Mimi Tullo namjua Vizuri amekuja hapa
kuniharibia tu,najua wanachukia haya
mashindano ya Uhuru Marathoni kwa madai mashindano haya yangekuwa ya kwao
Riadha Taifa (RT) eti mimi nimeyapora mashindano haya kwao,na hata pia kwenye
Mkutano wangu na Waandishi wa Habari mimi nilimuita Mwandishi mmoja wa Tanzania
Daima ambaye ni Khadija Kalili na sio Mhariri na najua kaja kwa nia gani Tullo”alisema
Innocent.
Kwa upande wake Mdau wa Riadha nchini
ambaye aliwai kuwa mwanariaza nchini William Gidabudai alipotafutwa kuzungumzia
mtafaruku huo wa Viongozi wa Riadha alisema yeye amesikia kilichokuwa kinataka
kutokea kwenye mkutano na Waandishi wa Habari.
“Mimi
nimesikia kwamba Tullo Chambo na Suleiman Nyambui wanataka kupigana kiukweli
anachokifanya Tullo ni sahihi Lengo lake ni kutetea Haki na usawa kwenye Mchezo
wa Riadha na huyo Nyambui anafanya ubabaishaji tu kutaka kuharibu Mambo”alisema
Gidabudai.
Alipotafutwa Katibu wa Riadha nchini
Suleiaman Nyambui alisema naye alisema moja tu kwamba Mwandishi wetu amtafute Tullo
chambo ndio asema sio yeye.
Naye Tullo Chambo alipohojiwa na Kituo
cha Magic Fm kuhusu fujo hiyo alisema anachokidai yeye ni sawa kwani taratibu
hazikufuatwa na Nyambui kwani alifanya mambo kinyume na utaratibu.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni