Zinazobamba

HABARI ILIYOTIKISA JIJI--KAFULILA AIBUKA TENA UPYA,SASA AMVAA KIKWETE,SOMA HAPA KUJUA

Na Karoli Vinsent
     WAKATI Rais Jakaya Kikwete akisuasua kuwachukulia hatua viongozi waliotajwa na Bunge kuhusika Katika Wizi wa zaidi ya Bilioni 320 kwenye Akaunti ya Tegeta Esrcow ,naye Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila Ameibuka upya na Ameivaa Ikulu
       Na kusema Ikulu ya Rais Jakaya Kikwete inamedhamilia kuwalinda wezi waliohusika katika kuiba pesa hizo,baada ya kumzuia Mkurugenzi wa ofisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa PCCB Dk Edward Hosea kutoiwasilisha Taarifa ya uchunguzi juu ya sakata hilo la Esrcow  kwa Umma kutokana na Ripoti ya PCCB kuwataja vigogo wa Ikulu kuhusika katika kuchota pesa kwenye Benk ya Stabink.
    Hayo yamebuliwa mda huu Jijini Dar es Salaam na Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo Kafulila  huku akizungumza kwa uchungu alisema Inasikitisha kuona jinsi Ikulu inavyotumia ubabe wake kumzuia Dk Hosema kutoiweka wazi ripoti yake ya uchunguzi.


   “Tunafahamu wazi serikali inataka kuwalinda watu waliochota pesa,kutokana na kitendo chake kumzuia PCCB asiweka hadharani ripoti kwa kisingizia uchunguzi ujakamilika,ujakamilika kivipi wakati tunakumbuka wazi Mkurugenzi wa PCCB Dk Hosea wakati kongamano la SADC  kuhusu Rushwa  uliofanyika mkoani mwanza mwezi Novemba”
“Alisema ripoti yake ya uchunguzi kuhusu Akaunti ya Escrow umekamilika na tayari wameshamkabidhi Waziri Mkuu ingawa waziri huyo mkuu alikana,na hii yote inafanyika hivi ni kutokana na Ripoti ya PCCB kuwepo  na majina ya Vigogo wa Ikulu ambao walichota pesa kwenye Benki ya Stabink”alisema Kafulila
      Kafulila aliongeza kuwa leo majina ya watu waliochota pesa kwenye Benki ya Mkombozi tu wanatajwa ,huku wengine kwenye Benki ya Stabink Benki wakiachwa kwa kuwa ni vigogo wa Ikulu.
      “Leo majina ambao kamati ya PAC waliyopewa na PCCB ni ya Benki ya mkombozi huku majina ya Benki ya Stabink ambao watu walichota pesa kwa maboksi,Sandalusi,magunia ambao wengi wao ni vigogo wakubwa wa ikulu wakiachwa,na ndio maana Ikulu hii inakataza Ripoti ya PCCB iwekwe wazi kwakuwa itaweza kuvuruga nchi kwasababu wahusika waliochota pesa wengi ni watu wa Ikulu”aliongeza Kafulila.
    
 Kuhusu Jeuri ya Mmiliki wa IPTL Bwana Seith
       Kafulila ambaye  pia ni katibu Mwenezi wa Chama cha NCCR Mageuzi alisema Jeuri aliyekuwa nayo bwana Seith kwa kuzivimbia Mamlaka zote ikiwemo Mamlaka ya ukusanyaji Kodi TRA inatokana na kigogo huyo kufahamu wizi huo ameufanya na vigogo wa kubwa wanchi.

   “Huyu bwana seith anakuwa jeuri sana kwakuwa anauhakika pesa za Escrow amekula na wengi hata akifanya jambo anajua wazi hakuna wakumchukulia hatua kwakuwa wako wengi, na  hii inatokana kutokuwa na serikali makini ndio maana inamuacha huyo taperi kufanya anavyotaka ila serikali ijue huyo mtu avyojisifu hivi atakujakuleta machafuko nchini”alitabainisha Kafulila.
     
Katika hatua nyingine Mbunge huyo wa kigoma Kusini alisema kwa sasa chama chake cha NCCR kwa kushirikiana na Umoja wao wa Vyama vya upinzani nchini waanza Rasmi kwenda kwa wananchi kuwaeleza kuhusu suala nzima lilivyo la Escrow na Wamepanga kuanza na Mkoa wa Kigoma.
      
 “Tuanza tena ziara Mkoani Kigoma kuhamasisha Umma uelewe kuhusu Ufisadi huu,na tunatawajulisha Watanzania kuwa CCM haina uhalali wa kuchaguliwa kwasababu imeshindwa kuisimia serikali yake kwani Makam mwenyekiti Taifa na Katibu wa CCM wamesisitiza kuwa wahusika wawajibike lakini wamegoma”alisema Kafulila

Hakuna maoni