HIVI NDIVYO TGNP WALIVYOLIA NA UKATILI WA KIJINSIA BONGO
Mkurugenzi mkuu wa TGNP akifafanua jambo mbele ya ummati wa wanaharakati katika viwanja vya vyao, |
Na Karoli Vinsent
WITO umetolewa kwa Jamii kupinga
vikali Vitendo vya Ukatili wa Kijinsia kwa wanawake, Vijana pamoja na watu wenye ulemavu ili kuikomboa
Jamii kutoka kwenye Vitendo hivyo.
Rai hiyo imetolewa mda huu Jijini Dar Es
Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Bi Lilian Liundi wakati wa uzinduzi wa Kampeni
ya Wiki ya kupinga Vitendo vya Ujangili iliyoanza mwezi Novemba 25 mwaka huu
ambapo Be Liundi alisema kwa sasa jamii inachangamoto kubwa sana kuhusu vitendo
vya ukatili wa Kijinsia ambayo inaifanya
jamii kuishi katika hofu kubwa hususani wakina wanawake na vijana pamoja na
watu wenye Ulemavu .
Maandamo ya Wanafuzni Pamoja na Wanaharakati wakipinga unyanyasaji wa Kijinsia wakiwasili makao makuu ya TGNP Jijini Dar es Salaam picha na Suleiman Magari |
Bi Liundi alizidi kusema kuzinduliwa kwa kampeni hii inayoitwa Funguka,fichua ukatili kwa afya ya
Jamii,itatoa mwanya kwa jamii kuvunja ukmya kila wanaposhuhudia Vitendo
vinavyoanyilia unyanyasaji wa Kijinsia basi wachukue hatua.
Pia Alitabainisha kuwa hali ya vitendo vya
unyasaji wa kijinsia nchini vimeongezeka kwa kiasa kikubwa kwani kati ya
wanawake 2 kati ya 5 wamefanyiwa viendo vya ukatili wa kijinsia.
Vilevile Bi Liundi alisema Sababu ya
kuongezeka Vitendo hivyo vimetokana na
kuongezeka wa Shughuri hizo ambazo ni maeno ya usafirishaji haramu kwa wasicha,Tatizo la Ajira,Biashara
ya ngono pamoja na ndoa za utotoni .
Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la UNFPA nchini |
Kwa upande wake Kaimu mtendaji wa Tume
ya Haki za Binadamu na utawala Bora Tanzania Bi Mary Massay aliitaka jamii
kutovivumilia Vitendo vya Ukatili wa Kinjisia kwa kukalia na taarifa zinazohusu vitendo hivyo kwa kutoa
Taarifa kwenye Madawati ya Vitendo vya Kijinsia pamoja na Polisi.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni