HICHI NDICHO KILICHOWAKUTA YANGA LEO-FAIDI KWA PICHA
Kikosi cha timu ya Azam FC kilichoanza mechi ya leo.
Kikosi cha timu ya Yanga.
Wachezaji wa timu ya Azam FC wakishangilia goli yao la kwanza dhidi ya Yanga.
Mshambuliaji wa Yanga,Hamis Tambwe akiipatia timu yake bao la kusawazisha katika mtanange wa muendelezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam leo.Picha zote na Othman Michuzi.
Mfungaji wa goli la kwanza kwa timu ya Yanga,Hamis Tambwe na Mfungaji wa Bao la pili,Simon Msuva wakishangia ushindi wao dhidi ya timu ya Azam katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam hivi sasa.
Shangwe kwa Yanga.
Beki wa timu ya Azam, Pascal Wawa akimdhibiti Mshambuliaji wa Yanga,Hamis Tambwe katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara uliochezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo.
Benchi la ufundi la Yanga.
Makocha wakifatilia timu zao.
Mchezaji wa Yanga,Kpah Sherman akitoa pasi mbele ya mabeki wa Azam.
Beki wa kushoto wa Azam FC,Shomary Kapombe akiangalia namna ya kumdhibiti Simon Msuva wa Yanga.
Kapombe na Msuva......
Danny Mrwanda akipokea pasi mbele ya Beki wa Azam,Aggrey Morris.
Kiumbo mshambuliaji wa Yanga,Haroun Nyionzima akiruka daluga mardadi mbele ya mabeki wa Azam.
Nyomi la Yanga.
Mashabiki wa Azam wakishangilia Goli lao la kusawazisha.
Mrwanda akimtoka Beki wa Azam.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni