HABARI NJEMA KUTOKA TAMWA LEO--JAMII IMEANZA KUWA MWAMKO WA KIPINGA VITENDO VYA UKATILI-SOMA HAPA KUJUA
Pichani ni mkurugenzi wa Mtendaji wa chama cha Waandishi Wanahabari nchini TAWMA Bi Varelia Msoka akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Ripoti ya utafiti kuhusu ukatili wa Kijisia |
CHAMA cha Waandishi wa Habari wanawake nchini (TAMWA) Kimezindua Ripoti ya Awali ya Ukatili wa Kijinsia nchini na kuonyesha kuwa Jamii imeanza kuwa na uelewa Mkubwa kuhusiana na Masuala ya Ukatili,huku mila na desturi zikiendelea kuwa kikwazo cha mapambano hayo.
Hayo yamesemwa jana Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Mtendaji wa chama cha Waandishi Wanahabari nchini TAWMA Bi Varelia Msoka wakati wa Uzinduzi wa Ripoti ya Ukatili wa kijinsia nchini na kushuhudiwa na wadau mbalimbali ikwemo Waandishi wa Habari ambapo Bi Msoka alisema jamii imeanza kuwa na ulewa mkubwa juu ya mambo ya ukatili wa kijinsia tofautisha na miaka mingine kwani mwaka 2012 mwamko wa kupinga ukatili ilikuwa asilimi 56 huku mwaka huu mwaka 2014 ukiongezeka na kufikia asilimi 69.2.
Waandishi wa Habari wakifuatali kwa makini Uzinduzi huo wa Ripoti ya Utafiti |
"Hivi sasa kuna tatizo katika mahakama zetu na polisi katika kuendesha kesi hizi maana waliofanyiwa vitendo hivyo wanashindwa kuendelea kufuatilia kesi zao,baada ya kubainika kuwa kuna upindishwaji wa haki katika kesi zao zinazofanywa na vyombo vya mahakama na Jeshi la Polisi"alisema Bi Msoka.
Pichani ni viongozi wa Chama cha Waandishi wanahabari Tamwa wakipokea Ripoti hiyo |
Hakuna maoni
Chapisha Maoni