HABARI KUBWA LEO-UKAWA WAMBAMIZA KIKWETE,WASEMA MAZITO,DK SLAA AMVAA YEYE NA USALAMA WA TAIFA WAKE SOMA HAPA KUJUA........
Pichani ni Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahimu Lipumba Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam picha na Exaudi MTEI |
NA KAROLI
VINSENT
WAKATI wananchi
wakiwa bado hawajalizika kuhusu Hatua
alizochukua Rais Jakaya Kikwete, Juu ya maamuzi ya Bunge kuhusu ufisadi wa Zaidi
bilioni 306 kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow,kutokana na Rais Kikwete kulikejeri
Bunge kwa kuyatupia mbali mapendekezo mengi ya Bunge .
Nao Umoja wa Vyama vya vikuu vya
Upinzani nchini ambavyo vinaunda Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA
vimeibuka na kumvaa Rais Jakaya Kikwete na kusema anahusika kwa kiasi kikubwa
kwenye Ufisadi huo, kwa kitendo chake cha kumtetea Mmiliki wa wa kampuni ya Independent power limited (IPTL), Bwana Harbnder Singh (Singasinga)
Na Kusema Umoja huo utaanzisha Maandamano
nchi nzima kupinga Ufisadi huo ambao wanadai unalindwa na Rais Kikwete kutokana
na yeye kuhusika katika Wizi huo .
Kauli hiyo ya Vyama hivyo vikuu vya Upinzani
vinavyounda UKAWA umetolewa leo Jijini
Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Umoja huo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha
Wananchi CUF Profesa Ibrahimu Lipumba wakati wa mkutano na waandishi wa Habari
uliohitishwa Mahususi ili kuzungumzia hutuba ya Rais Kikwete kuhusu sakata hilo
ambapo –
Profesa Lipumba alisema inasikitisha
kuona Rais Jakaya Kikwete ameacha kulitetea shirika la Umeme Tanesco na
kuwatetea Mataperi wa IPTL ambao wameliingizia hasara la mabilioni ya Fedha
shirika hilo.
“Hutuba ya
Rais kikwete imekuwa mtetezi mkubwa wa Mmiliki wa PAP,anaacha kulitetea shirika
la umma la Tanesco,harafu anadanganya umma kwa kiasi kikubwa kusema kwamba pesa za
IPTL si za Umma hivi anashindwa hata kuelewa Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikal
CAG ambayo inaonyesha wazi kwamba
wamiliki hawa wamefanya utaperi wa wazi kabisa katika umiliki wake “
“Taarifa za mauzo ya Kampuni ya Mechmar
kwenda piper link kwenda PAP ziliwasilishwa katika taasisi mbalimbali za
Serikali na bwana Singh sote tunafahamu ni kughushi nyaraka ili akwepe Kodi na
hili ni kosa,hivi Kikwete alioni hili?”alihoJi Profesa lipumba.
Profesa lipumba alizidi kusema hata
Maazimio yanayotokana na Taarifa ya CAG yanaonyesha wazi kuwa PAP siyo mmiliki
wa harali wa hisa za Kampuni ya Mechmar lakini Rais Kikwete hakuliona hilo.
Pichani ni Dokta Slaa akizungumza na wanahabari leo |
Kwa Upande wake Katibu mkuu wa Muungano vyama hivyo wa Vya Upinzani
vinavyounda UKAWA ambaye pia naye ni Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo CHADEMA Dokta Wilbroad Slaa amesema Umoja umepanga kuzunguka nchi
nzima ikiwemo kuandaa maandamano kupinga kile wanachodai Rais Jakaya Kikwete
amewalinda wezi wa Ufisadi huo.
Dokta Slaa aliongeza kuwa Kitendo cha
Rais kikwete kuwatetea Wamiliki wa kampuni ya IPTL ni wazi Rais Kikwete
anahusiki kutokana na kuwepo kwa ushahidi wa yeye kuhusika na Wezi huo.
“Tunajua wazi kwamba Rais kikwete kuhusika
na wizi huu kwani kunamtu mmoja anaitwa Guruma ambaye katika watu waliopewa pesa na
bwana James Rugimalira jina lake limetajwa kupokea mabilioni ya Fedha na mtu
huyo mimi namfahamu sana,Bwana Guruma anajulikana sana ni msimamizi wa Miradi
ya Rais kikwete na leo kachukua pesa za Escrow unategemea nini hapa na ndio
maana anasuasua kuwachukulia hatua wamiliki wa IPTL”Alisema Dokta Slaa.
Aidha,Dokta Slaa alisema kitendo cha Ufisadi
huo kutokea na Idara ya Usalama wa Taifa
kushindwa kulinda nchi kwenye ufisadi
huo ni wazi idara hiyo imeshindwa kazi.
“Usala wa Taifa upo kila Barozi inashangaza
sana kuona Idara hii inashindwa kuona utaperi wa mmiliki wa IPTL au tutegemee
nini ndio maana hata kwenye Ufisadi wa EPA,tuliona Jinsi Kampuni iliyokuwa
ikimilikiwa na Ofisa wa Usalama wa Taifa ilivyochota pesa unategemea nini”
“Na hata Kikwete alivyosema mara baada ya kutua
uwanja wa ndege alipotoka kutibiwa anavyosema
alijui sakata hili kutokana na yeye kuwa kwenye matibabu , ni kuwadanganya watanzania kwani
baada ya masaa mawili kutoa uwanja wa ndege hapo,niliona email aliyekuwa akitumiana na
bwana Rugimalira,sasa huyo ni kiongozi kweli”alihoji Dokta Slaa.
James mbatia |
Naye Mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi
James Mbatia alisema ni Rais kikwete amekosa maamuzi katika nchi kutokana na
kitendo chake cha kushindwa kuwachukulia hatua waliohusika na kusema pesa za
wananchi zimepotea huku taifa likiosa fedha hususani wao wabunge mapaka sahivi hakuna hata mbunge aliyepata hata mshahara.
Umoja huo wa UKAWA ni muunganiko wa
Vyama vya CHADEMA,CUF na NCCR pamoja NLD.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni