HABARI KUBWA LEO-MAZITO YAFICHUKA YA PROFESA TIBAIJUKA KUFUKUZWA KAZI KWAKE,ALIONYESHA USHUJAA MBELE YA KIKWETE,SOMA HAPA KUJUA
Pichani ni Profesa Anne Tibaijuka Picha na Maktaba |
NA KAROLI
VINSENT
WIKI moja Kupita Baada ya aliyekuwa Waziri wa
Kazi,Nyumba na Mandeleo na Makazi Profesa Anna Tibaijuka kufukuzwa kazi kwenye
nafasi hiyo,sasa Mengine mapya yaanza kufichuka kuhusu kufukuzwa kazi kwake,MTANDAO HUU umeelezwa.
Taarifa Zinasema Prof Tibaijuka alifukuzwa
kazi kutokana na ukosefu wa Maadili kama
ambavyo Rais Jakaya Kikwete alivyodai,
Rais Kikwete alitangaza kumfukuza kazi
Mbunge huyo wa Muleba Kusini (CCM)katika Mkutano wake wa Wazee wanaokaa mkoa wa
Dar es Salaam uliofanyika Mwanzoni mwa wiki liyomalizika jana Jijini Dar Es
Salaam,ambapo Rais Kikwete alisema Waziri huyo alipokea zaidi ya Bilioni 1.6
kutoka kwa Mbia wa Kampuni ya IPTL,Bwana James Rugimalira ambapo ni Kinyume na
Maadili ya utumishi wa Umma.
Licha ya Profesa Tibaijuka kujinadi
katika Mkutano wake na Wandishi wa Habari aliouhitisha Alhamisi ya Wiki
iliypita na Kujinadi kwamba hawezi kujiuzulu kwenye Nafasi ya Uwaziri kwa Madai
hakuhusika kwenye wizi wa zaidi ya Bilioni 306 kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow
iliyokuwa BOT.
Taarifa za Kuminika ambazo Mtandao huu
umezipata zinasema Shinikizo la kufukuzwa Prof.Tibaijuka limepewa nguvu na
baadhi wa makada kutoka ndani ya chama cha Mapinduzi ambao wanamwona tishio
katika harakati zake za kutaka kumrithi Rais anayemaliza mda wake Jakaya
kikwete mwakani 2015.
Kwa Mujibu wa Chanzo chetu cha
kuaminika kinasema Profesa Tibaijuka alikutana na Rais Kikwete Ikulu Jijini
hapa siku ya Jumatano iliyopita.
Ambapo katika mazungumzo yake Mtoa
taarifa huyo anasema Prof Tibaijuka alimueleza Rais Jakaya Kikwete Hatua kwa
hatua jinsi Fedha zilivyotolewa na Rugimalira hadi kupelekwa kwenye Akaunti ya shule ambayo ipo katika Benki ya
M,Sea View iliyoko Jijini Dar Es Salaam.
Aidha,katika Kikao hicho Rais Kikwete
alikubaliana na Prof Tibaijuka na akamtaka akaitishe mkutano na Waandishi wa
Habari ili kutoa ufafanuzi wa jambo hilo.
Na ndivyo Prof Tibaijuka akaitisha mkutano wake na Waandishi wa Habari katika
Hoteli ya Hyatt Regency (KILIMANJARO)
Akilielezea hilo Ofisa mmoja wa Ikulu
alinukuliwa na chanzo kimoja cha Habari alisema baada ya kukutana na waandishi
wa Habari, aliitwa tena Ikulu,safari hii alikutana na Makamu wa Rais Dk,Mohamed
Gharib Bilali na Waziri Mkuu mizengo Pinda.
“Walipofika
hapa Ikulu,Prof Tibaijuka alikutana na
Rais Kikwete Dk Bilali na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakamwambia kuwa Jinsi hali
ya Hewa ilivyochafuka ni vema akawapisha kwa kujiuzulu yeye alikataa”
“Akasema
hawezi kurudi tena kwa wananchi kuwambia anajiuzulu kufanya hivyo ni kugeka
jiwe ,kama wao wanamwona afai,basi wamfukuze kazi lakini siyo kujiuzulu”aliileza Ofisa huyo
Mwandamizi wa Ikulu ambaye akutaka Jina lake litajwe mtandaoni
Mbali na hivyo Taarifa Zengine ambazo
Mtandao huu unazo pamoja na Nyaraka mbalimbali zinamwonyesha Profesa Tibaijuka
akipigania Uwaziri Tangu Sakata hili lilivyokuwa Bungeni,lakini viongozi wa Bunge
wakiongozwa na Spika Anne Mkinda walimyima haki hiyo ndio maana Rais Kikwete
alipogundua kwamba Bunge lilimyima haki ya Kujitetea ndipo akamtaka akajitete
kwa wananchi.
Akiandika kwa Spika Makinda tarehe 20
Novemba 2014 Prof Tibaijuka alisema “Pamoja
na kuomba kuchangia kupitia Mhe Jestina
Muhagama –Katibu wa Bunge wabunge wa CCM-hadi sasa hakuna uhakika kama nitapewa
nafasi hiyo kabla hojakufungwa’
Barua hiyo kwenda kwa Spika Makinda
ilikuwa na kichwa cha Habari hivi “Muda
wa Kujitetea mbele ya Bunge kufuatana a kutajwa kwa jina langu katika Taarifa
ya PAC –Issue ya Escrow
Katika kile kinaoneka ni kwamba Spika
Makinda alikuwa anataka kumsulubu Msomi huyo alimjibu “ Suala hili ni
kubwa sana,maelezo yako hapa Bungeni
hayataweza kukupa haki ambayo unastahili”
Alisema “Ushauri wangu jiandae Vizuri kusudi
vyombo vitakavyoshughulikia , vikikuita
uweze kujitetea ufanye hivyo,sio humu ndani”
Barua hiyo ya Anna Makinda ambayo
ilimjibu Prof Tibaijuka aliandikwa Novemba 28 mwaka huu ina na Kumb
Na.CBC.155/188/02/16
Hata hivyo Profesa Tibaijuka
hakukubaliana na majibu ya Makinda akandika tena barua nyingine siku
hiyohiyo,Profesa Tibaijuka akasema “Asante kwa kujibu barua yangu.Ninakusihi
sana unipe muda kuchangia kama unanitakia kheri katika maisha yangu .Dunia
inasubili Kauli Yangu”
Licha ya kulalamika hivyo Spika Makinda
akajibu Andishi hilo kwa kusema “Mh Prof,Tibaijuka,Bunge hili haliwezi
kukusaidia.Naomba ukubali kujiandaa kwa hatua nyingine.maana wataibua hata
mambo hayapo humu .Naomba unisikilize”
Habari zinasema Mbali na madai hayo
Prof Tibaijuka amekuwa katika wakati mgumu na Baada ya kukatalia Bodi ya
wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)kumlipa mshahara wa dola marekani 19,000 (elfu kumi na tisa kwa mwezi)
karibu zaidi ya Milioni 32.3 milioni mkurugenzi wa Shirika hilo Nehemia Msechu.
Bodi ya NHC iliyoidhinishwa mshahara wa
dola 19,000 kwa mwezi inaongozwa na mbunge wa kuteuliwa Zakia Meghji.
Kwa sasa
Msechu anaweka kibindoni dola za 11oo0 zaidi ya milioni 18 pamoja namrupumrupu
mengine kedekede.
Fedha hizi
ziliidhinishwa na Pro Tibaijuka na kwenda kinyume na Bodi ya Shirika
hilo,Wadadisi wa Mambo wanasema kufukuzwa na kwa Waziri huyo kumeleta haheni
kwa Bodi ya NHC kufanya anasa ya Fedha za Umma.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni