UTAFITI--HAKUNA KAMA LOWASSA NDANI YA CCM,CCM YAONYWA,WASEMA WAKIBUGI TU CHAMA KITAMEGUKA SOMA HAPA KUJUA
Utafiti mpya ambao matokeo yake yamepangwa kutangazwa rasmi leo jumatano hii, umeonyesha kwamba endapo uchaguzi mkuu wa Rais wa JMT ungefanyika hivi sasa, Mbunge wa Mondlu, Edward Lowassa angeibuka mshindi. Twaweza imemaliza utafiti wake, matokeo yatatangazwa Dar es Salaam leo. Ndani ya CCM Lowassa alishindanishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe, Waziri wa Africa Mashariki Samwel Sita, Waziri wa Katiba na Sheria Dk.Asha Migiro, Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli na waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Katika hatua nyingine utafiti uliofanywa na wahitimu wa chuo kikuu cha Dar Es Salaa kwa wajumbe wa Baraza la Umoja wa Vijana (UVCCM) katika kikao kilichoketi juzi Dodoma, Lowassa aongoza tena....
Baada ya mkutano wa Baraza la umoja wa vijana CCM kumalizika, sasa ni wazi hakuna wa kumzuia Lowassa kuingia Ikulu. Baada ya kikao cha NEC mwezi uliopita nilisema kuwa katika hii safari ya kuingia ikulu Lowassa kafika katika mitaa ya IFM ila baada ya huu mkutano wa vijana wa UVCCM walai kwa sasa Lowassa ni Rais na kashafika katika jengo la wizara ya elimu, adjacent na ikulu zikiwa zimebaki mita chache tu aweze kuingia ndani.
utafiti uliofaywa na wahitimu wa chuo kikuu cha Dar es Salaam kwa wajumbe wa baraza kuu la vijana uvccm. Utafiti huo ulihusu hasa kujua ni nani vijana hao wa chama tawala wanaona anafaa kwa kuongoza nchi 2015; na pili ililenga kuwahoji kuhusu katiba pendekezwa kama wanaona inafaa ipigiwe kura kabla ya uchaguzi mkuu au baada ya uchaguzi mkuu wa 2015. Kwa kuanza na objectice ya kwanza ya kujua nani anafaa kuwa rais wa 2015 kwa kura za wajumbe hao ni kama ifuatavyo…….(Note jumla ya wajumbe wa baraza kuu la vijana ni 150, na huu utafiti uliweza kuwahoji wajumbe 60 kwa maana ya sample; njia kubwa iliyotumika ni dodoso au maarufu kama questionnaires)…..matokeo…..
1. Edward Lowassa alipendekezwa na wajumbe 42 kati ya hao 60 (68.8%).
2. Mizengo Pinda alipendekezwa na wajumbe 6 kati ya hao 60 (10%).
3. John Magufuli alipendekezwa na wajumbe 3 kati ya hao 60 (5%).
4. Dr Asha Migiro alipendekezwa na wajumbe 3 kati ya 60 (5%).
5. Frederick Sumaye alipendekezwa na wajumbe 2 kati ya 60 (3%).
6. Bernard Membe alipendekezwa na wajumbe 2 kati ya hao 60 (3%)
7. Mwigulu Nchemba na January Makamba wakapata kura 1 kati ya hao 60 (1.6%).
Katika huo mkutano kila kona uliyokiuwa unapita wajumbe wa baraza walisikika wakisema Lowassa atoshaa, Lowassa atosha, ukienda sehemu za migahawa ni Lowassa, ukienda maeneo ya jengo kuu la CCM ni Lowassa, ukienda kwenye bar mbali mbali Dodoma carnival, Nyerere Square, kisanju, Maisha club kwa kifupi kila kona ilikuwa jina la Lowassa. Huu ni utafitit uliotoa hamasa, umoja na matumaini mapya katika safari ya matumaini kwa watanzania, naomba niwaambie mlango wa rehema bado uko wazi kwa ajili ya kujiunga na kundi hili la ushindi, mtu asikudanganye na ukadanganyika hakuna kundi la ushindi zaidi ya kundi hili, ni wajibu wako kuwahi haraka ili upate kuhesabiwa na wewe.
Katika kubadilishana mawazo na wajumbe wa baraza la vijana nilipata wasaha wa kusikiliza ujumbe alioutoa mzee wango John Shibuda, kwa kweli huyu mzee amejaa busara ya hali ya juu.
Shibuda aliwaeleza vijana ya kwamba “unaweza kuwa na fedha za sarafu nyingi sana zenye kelele lakini hazina maana, na mwingine akawa na noti moja tu ambayo haina kelele ila ina maana kweli kweli”, tafsiri yake ni kwamba kuna wagombea wengi kweli kweli wakipiga kelele kama fedha za sarafu ila hawana maana na hili ni lile kundi waliokwisha jitangaza huku wengine wakienda Uingereza kupiga kelele zao za kutangaza nia kugombea urais (Kuna clip iliyopata umaarufu ya professor PLO Lumumba wa Kenya anashangaa viongozi kupeleka watoto wao kusoma nje, anashangaa wananchi na viongozi wa leo wakikimbilia kwenye mabalozi ya nchi za magharibi kupigania green card pasipo kujua kuwa wanaenda kuwa watumwa kwa mara ya pili, sasa hili swala la viongozi wetu kwenda kutangaza nia ya kugombea urais wakiwa ulaya kwenye vyombo vya habari vya wakoloni ni wazi huu ni utumwa uliopitiliza na kamwe tuwaogope kama ukoma viongozi wa namna hii).
Kuna wagombea wengine walipiga kelele za sarafu kwa kubebwa na WAMA organization lakini kadri siku zilivyozidi kwenda bila shaka iligundulika kuwa mgombea mwenyewe bwana Membe Bernard ana uwezo mdogo sana kupita kiasi, ndiyo mana kila kukicha kambi yake inazidi kubomoka na kwa taarifa za uhakika saizi kabaki na watu 3 tu ambao ni Nyalandu mume wa Aunt Ezekile, Prince na Richard Kasesela wengine wote wamekimbia.
Kundi lingine lenye kelele ni hili kundi linalojiita vijana, hili kundi kelele zao zinakera sana sana katika jamii na kwa wenye busara kama sisi ocampo four ni mara mia kuangalia katuni za Ben ten au Dora kuliko kusikia kelele za hawa wanaojiita vijana, eti January Makamba naye anataka urais, eti Mwigulu naye anataka urais, hahahahahaha eti na Kwigwangala naye anataka urais, kwenye biblia hawa ni sawa sawa na wale wanaopanda mbegu katika mawe. Kwa maneno hayo hapo juu Lowassa ndiyo fedha yenye thamani (noti), tena noti wekundu wekundu, Lowassa katulia, emekuwa akipuuza uongo na matusi za wahuni na wakora wa nchi hii, kwa kipindi kirefu Lowassa amekuwa jasiri, mpole, kiongozi mkakamavu, mwenye upendo na aliye jaaa tabasamu la furaha.
Tafsiri pana za hizo data zinaweza kuainishwa na kukataliwa kwa waziri mkuu Mizengo Pinda kuwa naibu kamanda wa Umoja wa Vijana, kitendo kilichopelekea Masaburi kufukuzwa kwenye nafasi ya kampeni meneja baada ya kutumia million 400 huku matokeo yakiwa zero (hata ingekuwa mimi lazima ningekasirika sana sana). Na pili haya matokeo kwa upana wake yanaweza kueleza hata kwa nini mchumia tumbo namba moja wa UVCCM na aliyekuwa rafiki mkubwa wa Rizone (kwa sasa ni paka na panya) kukataliwa kuwa naibu katibu mkuu bara na huyu siyo mwingine bali ni bwana Salum Hapi. Kwa sasa huyu bwana kahamia kwa Pinda baada ya kuona kumuuza Membe ni sawa sawa na kuhamisha mbuga ya Serengeti na kuileta Samora Avenue.
NB: Watanzania huu siyo wakati wa kucheza, 2015 siyo wakati wa kucheza, wenzetu wamekuwa wakipiga hatua kumi mbele kwa muda wa miaka hiyo yote, hivyo ili kuwakamata na kwenda nao pamoja sisi kuanzia 2015 tuwatafute viongozi wakutupaisha kimaendeleo, kiongozi mwenye maamuzi magumu siyo tu ndani ya nchi ila hata nje ya nchi ili tusiruhusu ukoloni kwa mara nyingine tena, na huyo sii mwingine zaidi ya Lowassa, tafadhalini sana sana tujitahidi na tuhakikishe hatufanyi makosa na tusije tukajutia katika huo uchaguzi ujao……………
Kuhusu objective ya pili, wajumbe wote 60 waliohojiwa waliona inafaa katiba inayopendekezwa ipigiwe kura kabla ya uchaguzi mkuu wa 2015 kama ilivyopangwa.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni