MATUMZI YA KONDOM KWA VIJANA YAONGEZEKA,SERIKALI YASEMA ITASAIDIA KUPUNGUZA MAAMBUKIZO MAPYA YA UKIMWI
Na Karoli
Vinsent
SERIKALI
imesema idadi ya vijana wanaotumia kondom imeongeza kwa kiwango kikubwa
tofautisha na miaka mingine,na kusema ongezeko hilo limesaidia kupunguza
mambukizo mapya ya virus vya Ukimwi nchini.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam
na Mratibu wa Uzazi wa Mpango kitaifa
kutoka wizara ya Afya nchini bwana Mouris Hiza,wakati wa semina kwa wadau
mbalimbali wa mambo ya afya ambapo seminia hiyo iliyoandaliwa na Kampuni isiyo
ya kiserikaliya DKT International inayoshugulika kutoa elimu kuhusu uzazi wa Mpango,ambapo alisema hali ya sasa ya matumizi ya kondom
hususani kwa vijana imeongezeka kwa kasi.
“Kiukweli hali
ni inaridhisha sana na jitihada hizi za maongezeko ya matumizi ya Kondom kwa
vijana imetokana na kazi nzuri iliyofanywa na Wizara ya Afya pamoja na Taasisi
mbalimbali za kupambana na Virusi vya ukimwi,na hii imetokana na vijana wengi
kutumia kondom katika kuzuia mimba na ukimwi nah ii ni jamba jema”alisema Hiza
Kwa upande
wake Meneja Masoko wa Kampuni hiyo isio
kuwa ya kiserikali ya DKT Davis Kambi alisema ni wakati umefika kwa serikali
kutoa elimu kwenye kwa watanzania kuhusu umuhimu wa uzazi wa mpango kama
Taasisi hiyo inavyofanya.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni