NI URAIS WA RUSHWA NDANI YA CCM,SIRI ZA VUJA MKUTANO WA UVCCM WASAKA URAIS WAMWAGA PESA HOVYO HOVYO,PINDA ATUHUMIWA SOMA HAPA KUJUA
Wakati kikao cha baraza kuu UVCCM taifa kikiendelea hapa mjini Dodoma wajumbe wa kikao hicho waanza kurambishwa asali ya mfuga nyuki Waziri Mkuu Mizengo Pinda, OKELLO kama kawaida yangu huwa sikurupuki hata kidogo ninacho kujuza ndicho kinachojiri katikati ya mji mkuu.
Waziri Mkuu mizengo pinda amemwaga kiasi cha fedha takribani tsh 50 millioni katika baraza la vijana UVCCM kwa ajili ya kusukuma ajenda zake za Urais 2015, kiasi hicho cha fedha kilikabidhiwa jana kupitia kwa mwenyekiti wa vijana mkoa wa Katavi Bwn. Kelvin Mbogo akishirikiana na mwenyekiti wa vijana UVCCM mkoa wa Dar es salaam Bwn.Said Matulanga, baadhi ya mambo ambayo ni ya kimkakati yanatarajiwa kusukumwa kupitia kiasi hicho cha fedha ni;
1.Kuhakikisha bwana Salim Ally Hapi anakuwa naibu katibu Mkuu bara ili aweze kuongeza timu ya watu ambayo itaweza kumsemea na kuongeza ushawishi wa Mizengo Pinda katika jumuiya ya vijana kama ilivyo pangwa tarehe 04/11/2014 katika ukumbi wa Lukas Bar maeneo ya Masaki jijini Dar es salaam
2.Kuwashawishi vijana wengine Wa Baraza kuu la Vijana kutoka katika kila mkoa kwenda kumsemea kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu Wa CCM Taifa na wapiga kura wengine katika kufanikisha malengo yake ya Urais 2015. Zoezi hili liliendeshwa maeneo ya Dodoma Carnival karibu na stendi kuu ya mabasi Dodoma mjini, kikao kilichoongozwa na Mwenyekiti wa vijana kutoka Mkoa wa Katavi ambapo baada ya baadhi ya wadau hao kupokea pesa hizo walianza kula raha ndani ya Club Maisha kuanzia majira ya saa saba usiku huo. wakiongozwa na kijana Dallas ambaye anaesemekana ni moja ya vijana wanaofanya biashara haramu ya madawa ya kulevya ambaye kwa sasa ni moja ya vijana wanaoratibu kwa karibu harakati za uraisi za Mizengo pinda..
OKELLO kwa kuipenda nchi yangu nitaendelea kukujuza kila hatua ya mchezo huu mchafu unao endelezwa na hii timu na timu nyingine yeyote ile kwani ni hivi karibuni mfuga nyuki huyu alijinasibu kuwa yeye ana millioni ishirini na tano (25) katika akaunti yake na jana katika kipindi cha bunge cha maswali ya papo kwa papo alipo ulizwa kuwa bado ile akaunti yake ina millioni 25 kwa aibu na fedheha aliinama chini mbele ya luninga huku akikosa majibu kiasi cha kuwafanya watanzania tuamini shutuma za ubadhilifu wa pesa ya umma kupitia ESCROW ACCOUNT na zile safari za Ulaya na Uarabuni sasa zimeonyesha matunda kwa kutunisha mfuko wake unaotumika vibaya kuwashawishi wana CCM na Watanzania kwa ujumla Kwa njia ya rushwa ya kimya kimya ili kumuunga mkono katika harakati zake za kuwania Urais
Chanzo ni Jamii Forum
Hakuna maoni
Chapisha Maoni