IKULU YA RAIS KIKWETE YAWANUNUA WATANGAZAJI HAWA WA TV,LENGO NI KUIPIGIA DEBE KATIBA ILIYOPENDEKEZWA SOMA HAPA KUWAJUA
Na Karoli
Vinsent
KATIBU mkuu
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Dokta Wilbroad Slaa amefanikiwa
kupata waraka kutoka ndani ya Ikulu ya Rais Jakaya Kikwete ambapo Waraka huo unaonyesha ikulu kutenga kiasi cha Sh Bilioni 2.5 kwa ajiri ya kuvionga vyombo vya Habari na
waandishi na watangazaji ili kuipigia Kampeni Katiba ilyopendekezwa ili wananchi waipigie kura ya ndio,
Waraka huo ambao mtandao huu unao unawaonyesha
watangazaji kutoka Tv mbalimbali nchini, ambao ikulu ya Rais Jakaya kikwete
imepanga kuwanunu ili kufanya kazi ya kuongoza vipindi mbalimbali nyenye lengo la kuwafosi wananchi waipigie
kura ya ndio wakati wakuipigia kura katiba iliyopendezwa.
Dokta Slaa aliufichua waraka huo juzi
Jijini Dar Es Salaam wakati wa mkutano na waandishi wa Habari Jijini Dar Es
Salaam ambapo Kwa mujibu wa Waraka huo kila mtangazaji wa kituo cha TV ambaye
ataongoza kipindi kimoja atapewa kiasi cha sh laki mbili (200000) kwa kila
kipindi ndani ya wiki 22 yaani katika wiki moja kipindi kitaruka mara mbili kwa
wiki na wananchi wataruhusiwa kupiga simu.
Waraka huo umewataja watangazaji wa vituo
vya TV ambao watanunuliwa, ni Natha Chingu ambaye ni Msimamizi wa Vipindi wa redio
ya East Afrika ambayo yeye atakuwa mtangazaji wakipindi cha Katiba ndani ya
Runinga ya EATV pamoja Samson Charlses kutoka kituo cha Tv EATV,
Kwa upande wa kituo cha Runinga cha ITV
watangazaji hao ni Abdallah
Mwipaya,Fatuma Nyangasa,Ramphedi Mwasako.Wote hao kutoka ITV
Waraka huo uliwataja watangazaji
wengine walionunuliwa kutoka Kituo cha Tv cha Chanel Ten ni David Ramadhani na
katika Shirika la Utangazaji la Serika TBC ni Shabani Kissu.
Pia Kituo cha Tv cha Star Tv ni Mzee
Angalieni Mpendu na Francic Mawalla na waraka huo umeshindwa kuwataja
watangazaji wa vituo vya ZBC pamoja Clauds Tv ambao wamenunuliwa ili kuipigia
kampeni katiba iliyopendekezwa,
Waraka huo ambao unaonyesha kila
mtangazaji atapewa Sh laki mbili kwa kila kipindi kitakachorushwa na wachambuzi
ambao watakua wanachambu kataba watapewa laki tano kwa kila kipindi.
Katibu Mkuu wa Chadema Dokta Slaa
aliwataka watanzania kuvipuuza vipindi hivyo pamoja na watangazaji hao kwa mdai
watakuwa wanafanya kazi tofauti na sheria za vyombo vya Habari.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni