HABARI ILIYOTIKISA JIJI-WAZIRI MWAKYEMBE NDIYE ANAYEKUMBATIA MAFISADI NDANI YA BANDARI,AMLEA MKURUGENZI
Na Karoli Vinsent
SIKU moja kupita baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulika na Hesabu za Mashirika ya Umma (PAC)
kufichua matumizi mabovu ya kifisadi ya zaidi sh bilioni 20 zilizotumika katika mkutano wa
wafanyakazi, matangazo na safari za ndani na nje za vigogo kinyume na taratibu
ndani ya Mamlaka ya Bandari nchini,
Naye waziri wa Uchukuzi Dk Harison Mwakyembe Ameingia kwenye Kasfa
Nzito ,kutokana na Kitendo chake cha kushindwa kumchukulia hatua,
pichani niKaimu mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA),Mzee Maden Kipande |
Kaimu mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA),Mzee Maden Kipande,ambaye
ameguza Mamlaka hiyo kuwa Genge la Ufisadi na kupelekea mabilioni ya fedha
kupotea.
Dk Mwakyembe,ambaye
anasifika kwa Wananchi kutokana
Uchapakazi wake na kutokuwa na Nidhamu ya Uwoga asiyemwogopa mtu
yeyote ,ambae atakuwa anavunja Sheria za Nchi, alikuwa anamwajibisha.
Lakini,mambo yamebadilika kwa Waziri hiyo,ambapo sasa ameonekana
ameshindwa kumchukulia hatua,Kaimu mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari
Kipande,kutokana na Vitendo vyake vya kifisadi huku vyombo vya Habari pamoja na
kamati za bunge kufichua ufisadi anaofanya.
Pichani ni WAZIRI wa Uchukuzi Dk Harison Mwakyembe |
Kwa Mujibu wa vyanzo vya kuaminika ambavyo mtandao huu umezipata kutoka
katika Mamlaka hiyo ambayo ni kitovu cha Maendeleo ya Nchi yetu amezipata ,zinasema mkurugenzi huyo amekuwa
akiwasimamisha wafanyakazi kinyume na Taratibu na sheria.
Chanzo hicho kinasema
mkurugenzi huyo,amekuwa akiwasimamisha watu tu pasipo kuwa na kosa lolote kwa
mfano miezi iliyopita ameanzisha Mpango
wa kumngoa Meneja wa Bandari ya Tanga,Hassani Kyomile eti akisema Meneja huyo
amekuwa akivujisha siri kwenye Gazeti moja la wiki akidai Mhariri wa
Gazeti moja la wiki ambalo limekuwa likifichua habari zake kwa madai mhariri
huyo ni Mhaya ,na meneja huyo pia nimhaya
anavujisha siri kwenye Gazeti hilo,
Ambapo kipande anaona
kumfukuza meneja huyo kutarahisisha mipango yake ya kifisadi pasipo kuvuja.
Chanzo hicho kilizidi
kusema Kipande amekuwa
akijivunia kwa Wanyakazi wake kwamba anaweza kufanya lolote na hakuna
wakumzuia,na amesimamisha watu kazi zaidi ya miaka miwili huku wakiwa wakipokea mishahara pamoja na
malupulupu wakiwa nyumbani bila hata ya
kufanya kazi.
Chanzo hicho kiliwataja wafanya kazi
hao,miongoni mwao ni Mama Muhindi,ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Masoko
TPA,ambaye alisimamishwa kazi na Kipande kwa Madai alikuwa anavujisha
siri(madudu)za TPA kuhusu kwenye vyombo
vya Habari,licha ya mkurugenzi
kipande alishindwa kutokea wala kukanusha kwenye vyombo vya Habari juu ya
Ufisadi huo ,
Tuhuma,zinginene
zinazozidi kumkabili kipande kuhatarisha usalama wa Bandarini kwa kutokuna na kutokuwepo na Kamera CCTV
pamoja na mita za kupima mafuta yanayoingia nchini kutokafanya kazi kwa miaka
mitatu sasa.
Jambo la kushangaza Mama huyo
Muhindi,alisimaishwa kazi tangu agosti 2013 na kipande,lakini hajahojiwa wala kurudishwa kazini ,huku
akizidi kuendelea kuchukua mshahara na Marupumarupu mengi bila kufanya kazi
hadi sasa wala hajahojiwa na mamlaka yeyote.
Chanzo,hicho kilizidi
kutaja orodha ya Wafanyakazi walionewa na Kipande ambae ni Mfanyakazi mwingine ndugu Msemo,aliyekuwa Afisa
Ununuzi,naye alisimamishwa kazi tangu agosti2013 kwa tuhuma zisizokuwa za
Ukweli wowote, lakini mpaka sasa naye anaendelea kuchukua mshahara pamoja na
marupurupu yote pasipo kufanya kazi.
Waliosimamishwa na
kipande kwa tuhuma hewa
Hery Arika,aliyekuwa Men eja Biashara wa Bandari ya Dar es
Salaam,alihamishiwa makao makuu na kuambiwa kuripoti idara ya utawala tangu
April 2013 hadi leo hii,Analipwa mishahara na marupurupu yake bila kufanya kazi
kwa mwaka mmoja sasa,kwa madai ya Kipande hamtaki.
Ajira za Upendeleo,
Kama kuna mgogoro unaofuka Moshi Ndani ya Bandari basi ni huu
unaotokana na Ajira za
Mhandisi Alois Matei,ambaye ni Naibu Mkurugenzi mkuu(Maendeleo ya
Miundombinu)na mhandisi William Shilla,ambaye ni mkurugezni wa
Uhandisi.Taharifa zilizopo zinasema kuwa Wahandisi hawa wawili
waliajiriwa na Kipande kupitia
Mlango wa Nyuma ,pasipo kufuata taratibu za
sheria.
Huu ni Mwenderezo wa
Unyama unaofanywa na Kipande ndani ya Bandari pasipo kuchukuliwa Hatua yeyote
kutoka kwenye Taasisi za Kupambana na Rushwa TAKUKURU,wala Wizara husika ya
Uchukuzi ambao,mamlaka hiyo iko chini yake.
Huku,Kipande
akinijinadi kwenye mkutano na Uongozi wa mamlaka hiyo,akisema mtu yeyote
atakaye pingana nae anamng’oa kwani yeye na mamlaka ya Bandari hawapati hasara yeyote bali
serikali ndio inapata hasara,na kama yuko mtu yeyete atakaye pingana
naye(Kipande )basi atamfukuza Kazi.
Duru, hizo zinasema mzee Kipande
amekuwa akifanya Vitendo hivyo vya Kifisadi huku akijinadi Hakuna mtu wa
kumng”oa nafasi hiyo kwa Madai,eti anajuana Kigogo mmoja aliyoko Ikulu ya Rais Jakaya Kikwete,ambae amekuwa
karibu na Kipande.Ndio maana Amekuwa akifanya Vitendo hivyo akijua hakuna mtu
wakumchukulia Hatua zozote.
Chanzo ni Gazeti la Jamhuli
Chanzo ni Gazeti la Jamhuli
Post Comment
Hakuna maoni
Chapisha Maoni