Zinazobamba

ALIYETUHUMIWA KUMTEKA DK ULIMBOKA AULA CHEO,DK SLAA AMSHANGAA JK,SOMA HAPA KUJUA



Na Karoli Vinsent
GAZETI la Mwanahalisi toleo lake la namba 302 la Jumatano Julai 18 hadi 21 mwaka 2012 na Toleo la namba 303 jumatano julai25 hadi agousti 1 mwaka huo,katika machabisho yake ilimtuhumu aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa (pichani) Jack Mugendi Zoka kuhusika katika kusimamia kitendo cha utekaji na utesaji alichofanyiwa Aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumiya ya Madaktari  Dk. Stephen Ulimboka ,
         Ambaye alitekwa, kuteswa na kutelekezwa kwenye msitu wa Mwabepande  ulioko Nje kidogo ya Jiji La Dar Es Salaam,ambapo mwili wake uliokutwa ukiwa na majeraha mwili mzima huku yeye akiwa atamaniki.
        Matoleo ya Gazeti hilo yaliituhumu Idara hiyo kuhusika katika Vitendo vya unyama na matoleo hayo yalimtaja Zoka kusimamia Vitendo hivyo.
        Katika hali ambayo ni ya kushangaza Rais Jakaya Kikwete amemteua Bw. Jack Mugendi Zoka kuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Canada.

             Bw. Zoka anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Alex Masinda, ambaye amestaafu kwa mujibu wa sheria uteuzi wake ulifanyika mwezi Semptemba mwaka huu.
        Na jana Rais Kikwete amemuapisha bwana Zoka kuwa Balozi nchini Canada,kupewa huku Ubalozi kumekuja baada ya kustaafu nafasi aliyekuwa nayo ya uandamizi ndani ya idara ya usalama wa Taifa.
      Kuteuliwa huku kwa bwana Zoka kumeibua manung’uniko kutoka kwa wanasiasa huku wengine wakihoji uteuzi wake kutokana na yeye kutuhiwa na vyombo vya Habari katika kuhusika katika kumtesa Dokta ulimboka.
       Akizungumzia uteuzi huo wa Zoka,Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Dokta Wilbroad Slaa wakati alipokuwa anazungumza na Mwandishi wa Mtandao huu kuhusu uteuzi huo, alisikitika sana na Kusema, Rais Kikwete akupaswa kumteua Zoka kwani ni mtu mwenye Rekodi ya utesaji na uuaji nchini.
     “Unamchagua mtu mchafu mwenye mipango ya Mauaji,mtu aliyepanga mauaji kwa kushirikiana na  kina Ramdhani Ighondu,eti unamteua kuwa Balozi da kweli nchi imefika pabaya,maana hana sifa”alisema Dokta Slaa.
       Gazeti la Mwanahalisi ambalo lilifungiwa na Serikali kwa mda usiojulikana kutokana na kufichua unyama huo ambao unadaiwa kufanya kwa idara ya usalama,
   Moja ya matoleo yalisema mipango hiyo ya utesaji ulipangwa na ofisa mmoja Usalama wa Taifa anayetajwa kwa Jina la Ramadhani Ighondu ambaye ni Mzaliwa wa Makole, Dodoma. Mfanyakazi wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS).
       Mbali na Kashfa hizo Zoka Hata hivyo, anakumbukwa zaidi kutokana na matukio mawili makubwa zaidi.
Hasa kitendo chake kama kiongozi wa juu wa Idara ya Usalama wa Taifa kwa kujitokeza hadharani na kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa.
      Tangu Tanzania kupata uhuru, ilikuwa haijawahi kutokea kwa kiongozi wa idara hiyo nyeti kujitokeza kuzungumza na waandishi wa habari.
     Zoka alijitokeza hadharani kwa mara ya kwanza Novemba 4,2010 alipoitisha mkutano na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) kutoa taarifa ya kukanusha tuhuma zilizoelekezwa katika idara hiyo na aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa.
        Taarifa hiyo ilikuwa ikikanusha madai ya Dk. Slaa kwamba maofisa wake wamekuwa wakihusika katika kuiba kura zake na kumwongezea mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM.
          “Tunasisitiza kwamba kwa makusudi au kwa kudanganywa na watu wanaojiita maofisa wa Usalama wa Taifa, Dk. Slaa amejikuta akitumia taarifa za uongo kutoa matamshi ya kuwadanganya Watanzania ili kuwachochea kuvunja amani. Kwa lugha ya kawaida tunasema Dk. Slaa ‘ameingizwa mjini’ na yeye ameingia kichwa kichwa,” alikaririwa wakati huo Zoka.
               Pia Zoka alijitokeza tena Julai 26, mwaka 2012 kujibu mapigo ya kuhusishwa kwa TISS na utekaji na utesaji wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Stephen Ulimboka na njama za kudhuru viongozi wa vyama vya upinzani.
            “Katika siku za hivi karibuni, kumejitokeza taarifa zenye tuhuma kadhaa dhidi ya Idara ya Usalama wa Taifa. Taarifa hizo zimekuwa zikitolewa kwenye vyombo vya habari zikiihusisha idara hii na matukio ambayo yanaidhalilisha na kuzua maswali mengi kwa wananchi.
        “Kati ya tuhuma hizo ni tukio la kutekwa kwa Dk. Stephen Ulimboka, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari na madai ya kufanywa kwa mipango ya kuwadhuru baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani,” alisema wakati huo.
          Akizungumzia uteuzi wake, Zoka alisema atahakikisha anasimamia maslahi ya Tanzania nchini humo.

“Ukizingatia Canada kwa sasa inatajwa kuwa miongoni mwa nchi ambazo uchumi wake unakua kwa kasi, hivyo nitahakikisha naangalia suala la uchumi la nchini humo linainufaishaje Tanzania,” alisema.

Hakuna maoni