TPSF YAITAKA SERIKALI KUWAPA FURSA WAZAWA KUWEKEZA KATIKA SEKTA YA USAFIRISHAJI, MENGI ASEMA WAZAWA WANAWEZA NA WASIBEZWE.. HABARI KAMILI SOMA HAPA
Serikali
imeombwa kuboresha miundombinu ya reli na kuiachia sekta binafsi
kuwekeza katika usafirishaji ,ikiwemo kununua mabehewa na vichwa ili
kufikia mpango wa matokea sasa (BRN) kwa haraka.
Akizungumza
jijini Dar es salaam mwenyekiti wa taasaisi ya sekta binafsi(TPSF)
Reginald mengi amesema kuwa ni muhimua sekta ya reli ikaboreshwa zaidi
kwa kuwa itasaidia kupunguza gharama hasa katika usafirishaji wa mizigo.
Mwenyekiti
huyo amesema kuwa watanzania wanauwezo mkubwa wa kuwekeza katika
kununua mabehewa na vichwa kama serikali itaweza kuwapa nafasi katika
kukamilisha mipango hiyo.
Bwana
Mengi aliongeza kuwa kwa sasa usafiri wa reli unachangamoto kubwa
kutokana na uchakavu mkubwa ambao unasababisha usafari huo usiweze
kusaidia kukuza uchumi wa nchi.
Mwenyekiti
huyo wa TPSF alishauri Serikali kuwapa mikopo sekta binafsi ili waweze
kushiriki kwa ufanisi katika kusaidia sekta ya reli nchini.
"Serikali
iweke mazingira mazuri kwa wawekezaji wa ndani kwani kwa kufanya hivyo
itasaidia kuongeza uchumi wa ndani na kuboresha hali zetu na kupunguza
umasikini kwa watanzania" amesema bwana Mengi
wakati
huohuo mkurugenzi wa sera na mipango wa wizara ya uchukuzi ndugu
Gabriel Migire amesema kuwa katika utekelezaji wa BRN wametoa kipaumbele
kuhakikisha reli na bandari zinafufuliwa.
Amesema
katika mpango huo wanakarabati reli ,wanaongeza mabehewa na injini ili
kuhakikisha mwaka 2016 reli isafirishe tani milioni tatu kutoka tani
200,000 za sasa.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni