RAIS KIKWETE ASHUSHULIWA NI KUHUSU KAULI YAKE YA KUWATAKA VIJANA KUGOMBANIA URAIS YAMPONZA SOMA HAPA KUJUA ZAIDI
RAIS Jakaya Kikwete, ameingia kwenye mvutano na makada wenzake kutokana na kauli yake ya kuwataka vijana wachague mgombea anayefanana na ujana katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwakani.
Wiki iliyopita akiwa mkoani Tabora, Rais Kikwete wakati akihutubia wananchi waliohudhuria kumbukumbu ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, sherehe zilizokwenda sambamba na kilele cha Wiki ya Vijana na hitimisho la Mbio za Mwenge wa Uhuru aliwataka vijana wachague mgombea anayefanana na ujana.
Alisema vijana ndiyo chachu ya maendeleo ya Taifa lolote hivyo washiriki katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi na kushiriki kupiga kura kumchagua rais anayefanana na kijana kama alivyokuwa yeye wakati akiwania nafasi hiyo mwaka 2005, wakati huo akiwa na umri wa miaka 55.
Katika vikao vya Halishauri Kuu (NEC) ya CCM viliyomalizika mwishoni mwa wiki mkoani Dodoma, Rais Kikwete alitakiwa asiingize udikteta katika mchakato wa kumsaka mgombea atakayerithi mikoba yake.
Mmoja wa wajumbe aliyekuwa kwenye kikao hicho Kilumbe Ng’enda, inadaiwa ndiye alikuwa mwiba mchungu kwa kumkabili Rais Kikwete ambapo alihoji kama mwenyekiti huyo ana mgombea wake mfukoni anayemuandaa ni vema akasema kuliko kutoa kauli za kushawishi kundi fulani lichaguliwe.
Mjumbe huo inadaiwa alisema alichokisema Rais Kikwete ni sawa kampeni ya kuwashawishi Watanzania hasa vijana kutowachagua watu wenye umri mkubwa jambo ambalo si sahihi.
Ng’enda inadaiwa alimuambia Rais Kikwete kuwa yeye ni Mwenyekiti wa chama hivyo hatakiwi kutoa kauli zinazoashiria kuwaengua mapema baadhi ya watu wanaotaka kuwania nafasi husika.
Katika kikao hicho Ng’enda alisema katiba, kanuni na taratibu za CCM zinatoa fursa kwa wanachama wote kuchagua na kuchaguliwa iwapo atakuwa ametimiza masharti ya nafasi anayoiwania.
“Kilumbe alimvaa Kikwete na kumuambia kuwa wagombea wanawania nafasi zao kwa kufuata katiba na kanuni za chama si kauli hivyo ni vema Mwenyekiti akaacha udikteta na kurusu demoktasia ichukue mkondo wake kwa kila mtu kuwania urais” kilisema chanzo kimoja.
Chanzo hicho, kilidokezwa kuwa kambi za wawania urais hasa zile zenye wagombea wenye umri mkubwa zilikerwa na kauli ya Rais Kikwete inayowaweka kwenye wakati mgumu wa kutimiza lengo la kuelekea Ikulu.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya kikao hicho licha ya hoja hiyo kuonekana nzuri lakini ilizimwa kwa madai kuwa kinachotakiwa kuangaliwa hivi sasa ni njia za kushinda uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Disemba mwaka huu.
Rais Kikwete, inadaiwa aliwataka wajumbe waache mjadala wa mbio za urais kwakuwa ajenda hiyo itajadiliwa katika kikao cha NEC kitakachofanyika Januari mwakani mkoani Mbeya.
Chanzo hicho kilizididokezwa wagombea wengi waliotangaza au kuonesha nia ya kuwania urais wana umri wa zaidi ya miaka 50 hivyo kauli ya Rais Kikwete inawaweka njia panda kutimiza ndoto zao.
Wanasiasa wazee wanaonekana kulengwa ni Fredrick Sumaye, Stephen Wassira, Edward Lowassa, Bernard Membe, Samuel Sitta, Mizengo Pinda.
Kauli ya Rais Kikwete ilitafsiriwa kulenga kuwabeba makada vijana kutoka CCM ambao ni January Makamba, William Ngeleja, Dk Hamis Kigwangalla, Mwigulu Nchemba na Dk. Emmanuel Nchimbi
Chanzo ni Gazeti makini la Tanzania Daima
Hakuna maoni
Chapisha Maoni