MAJANGA YAIKUMBA TIMES REDIO,TCRA YACHUKIZWA NA VIPINDI VYAKE ,SOMA HAPA KUJUA ZAIDI
Mwenyekiti wa kamati ya maudhui ya TCRA, Mhandisi Margaret Tabu Munyagi, akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari picha na Maktaba |
KITUO cha
Redio Times FM,kimetakiwa kulipa faini ya shilingi milioni moja baada ya
kukiuka sheria ya utangazaji kwa kurusha vipindi vya ngono muda ambao
haurusiwi.
Hukumu hiyo
ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na kamati ya maudhui ya utangazaji, katika
ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Margaret Munyagi.
Munyagi alisema
vipindi vilivyokiuka maadili hayo ni kile cha ‘Hatua Tatu’ kinachorushwa
kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 5 na kipindi cha mitikisiko ya Pwani
kinachorushwa saa 6 mchana hadi 10 jioni.
Akifafanua zaidi
makosa hayo, alisema katika kipindi cha ‘hatua tatu’, watangazaji katika
kipengele cha hatua za afya walikuwa wakiongoza mjadala wa mada ya kufanya
ngono mara mbili kwa wiki kunamwezesha binadamu kuishi muda mrefu.
Huku yule
anayefanya ngono mara moja kwa mwezi kuwa katika hatari ya kuishi muda mfupi.
Katika
mjadala huo, inaelezwa kuwa watangazaji walionekana wazi kushabikia ikiwemo
kuulizana wenyewe kuwa huwa wanafanya ngono mara ngapi, kitu ambacho ni kinyume
na maadili ya utangazaji kwa kuzungumza mambo hayo muda wa mchana.
Mwenyekiti
huyo alisema ni hatari kwa kuwa wakati huo wasikilizaji wengi ni watoto jambo
ambalo linaweza kuchangia kuzalisha kizazi kisichokuwa na maadili.
Wakati kwa
upande wa kipindi cha Mitikisiko ya Pwani, Mtangazaji alikuwa akizungumzia mada
ya msichana aliyefumaniwa baada ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mjomba
wake.
Kutokana na
makosa hayo alisema walisikiliza ushahidi kupitia CD za vipindi hivyo baada ya
kupata malalamiko kutoka kwa wasikilizaji na kujidhirisha kuwa walikuwa
wamekosea.
Pia alisema waliwaita upande wa walalamikiwa akiwemo Mkurugenzi
wa Times FM, Richard Nyaulawa na Mkuu wa Vipindi wa kituo hicho, Hemes Joachim,
ampapo wote walikiri makosa hayo.
Kwa mujibu wa
Munyagi faini hiyo watatakiwa wailipe ndani ya siku 30 kuanzia jana na imeenda
sambamba na onyo kali dhidi ya kituo hicho
Hakuna maoni
Chapisha Maoni