Zinazobamba

LICHA RAIS KIKWETE NCHI KUMUELEMEA KWA KIASI KIKUBWA,HAYA NDIO MAMBO MAZURI ALIYOFANYA KWENYE UTAWALA WAKE AMBAYO WATANZANIA HAWATASAHAU SOMA HAPA KUJUA ZAIDI

http://mtanzania.co.tz/wp-content/uploads/2014/07/Jakaya-Kikwete1.jpg

Na Karoli Vinsent
HUKU zikiwa zimebaki miezi michache tu ili Rais Jakaya Kikwete kumaliza vipindi vyake vya miaka kumi alivyokuwa mpangaji wa ikulu,hayo ndio mambo mazuri ambayo yatamfanya akumbukwe daima kwenye utawala wake
1. Ujenzi wa Sekondari za Kata ni maamuzi sahihi ingawa yana changamoto zake zinazoweza kutatuliwa na watakaomfuatia, lakini hapa JK ametumia madaraka yake vizuri


2. Ameendelea na uendelezaji wa Miradi ya Barabara, suala lililoanza kujitokea wakati wa awamu ya 3, JK ameendelea nalo suala hilo kwa kasi kubwa na kwa kipindi chote


3. Daraja Kigamboni, Malagarasi na Kilombero ni miongoni mwa mambo yatakayokumbukwa forever


4. Ongezeko la Taasisi za Elimu ya Juu limefanyika vizuri sana katika awamu ya Kikwete, mbali na UDOM lakini taasisi na vyuo vingi vimeimarishwa, kupandishwa hadhi na vyuo vingi binafsi vimeanziswa. Kwa sasa Taifa haliko tena na dhana ya UDII, Mzumbe na SUA. Aidha ari na moyo wa watanzania kulipia huduma za elimu umeongezeka.


5. Kumekuwa na ongezeko kubwa la ajira ukilinganisha na awamu mbili zilizomtangulia. Mkapa aliendesha Serikali nyembamba, suala ambalo ni zuri lakini lina changamoto zake kwa wale waliokuwepo wameliona hata akapewa sifa ya mzee wa "ukapa"


6. Mradi wa Bomba la Gesi kutoka Mtwara kwa lengo la kutatua kero ya Umeme ni hatua nzuri ambayo haijawahi kufanywa katika awamu ya 2 na ya Tatu (Vyanzo vya Nishati)


7. Mradi wa Ujenzi wa Kiwanda cha Chuma (Kule Liganga?) ambao maandalizi ya ujenzi wake yamekamilika ni hatua nzuri ili kuvutia au kuanzisha uwekezaji wa zana za Chuma pamoja na Viwanda vikubwa.


8. Hatua ya Kujenga Bandari mpya eneo la Bagamoyo yenye hadhi ya 4th Generation ni tukio litakalokumbukwa na vizazi Dahri vijavyo.


9. Hatua ya Utekelezaji wa mradi wa DRT ambao ulikuwepo miaka mingi pia ni miongoni mwa mazuri yaliyotendeka katika awamu ya JK


10. Zoezi la kutambua na kuwarudisha kwao wahamiaji haramu pia ni zoezi zuri ambalo bila shaka halijawahi kufanywa katika uongozi wa awamu nyinginezo kwa kiwango na utashi wa namna hiyo


11. Kitendo cha utekelezaji wa mradi wa vitambulisho vya Taifa ni credit kubwa kwa JK ambao hakuna sababu za wazi kwanini nchi imekaa miaka 50 pasipo na vitambulisho vya uraia kwa wakazi wake na raia wake


12. Ameendelea kuiweka Tanzania kwenye mahusiano mazuri kimataifa hususan SADC, UN na nyanja nyingine za Kitaifa. Ukiacha EAC ambayo sababu za kuzorota kwake ziko wazi, lakini maeneo mengine ame-play well.
picha; maendeleo ya ujenzi wa daraja la kigamboni eneo la kurasini jijini dsm. ujenzi ulikuwa asilimia 47 mwezi july

Hakuna maoni