HAWA NDIO MAASKOFU WA KANISA KATOLIKI DUNIANI WANAOTETEA USHOGA SOMA HAPA KUWAJUA
Hatua ya pamoja kuwaunga mkono makasisi watatu kwenye mitandao ya kijamii ndilo limekuwa gumzo kubwa kwenye mitandao hiyo nchini Chile wiki hii.
Yote haya yalianza na ujumbe kwa kiongozi wa kanisa katoliki Papa Francis.
Mnamo siku ya Jumapili, jarida moja nchini Chile liliripoti kuwa askofu na kadinali wa Chile ,Ricardo Ezzati, alituma ujumbe wa siri akilalamikia Vatican kuwahusu makasisi watatu, Felipe BerrÃos, Mariano Puga na José Aldunate.
Watatu hao wanajulikana vyema sana nchini Chile kwa kukosoa viongozi wa kanisa katoliki nchini humo na kuwaunga mkono wapenzi wa jinsia moja pamoja na kuunga mkono haki za wanawake kutoa mimba.
Duru zinasema kuwa vitendo vya makasisi hao vinachunguzwa na Vatican.
Neno "Ezzati" likaanza kuzungumziwa sana kwenye mtandao wa Twitter Jumapili wakati jarida moja lilipochapisha ripoti hizo. Neno hilo lilienezwa na kuenezwa zaidi ya mara 10,000 kwenye mtandao huo.
Wengine waakanza kulitumia kwenye Facebook.
Inaonekana matamshi mengi yanatoka kwa wananchi wa Chile wanaounga mkono makasisi hao watatu.
"Ezzati anaunga mkono msimamo wa kanisa dhidi ya wapenzi wa jinsia moja. Wanaompinga wanatetea utu,'' ulisema ujumbe mmoja kwa Twitter.
Ikiwa Ezzati atajaribu kulalamika kuwahusu makasisi BerrÃos, Puga na Aldunate kwa Vatican, wakatoliki wenye akili timamu, wanapaswa kulalamika kumhusu Ezzati,'' alisema Pablo Simonetti kupitia Twitter mwandishi mashuhuri nchini Chile na mmoja wa watetezi wa haki za wapenzi wa jinsia moja.
Wengi waliowatetea makasisi hao wanataka uwazi kutoka kwa kanisa ikiwa watachunguzwa na wanataka mazungumzo na viongozi wa kanisa.
Luis Larrain, mkuu wa kikundi cha kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja alisema kwa mzaha kwamba mmoja wa makasisi hao anapaswa kuateuliwa kuwa askofu mkuu wa Chile.
Aliongea na BBC na kusema Ezzati anachukiza kwa sababu wao wanajaribu kuanzisha mazungumzo na kanisa na anahofia kwamba matamshi kama haya yatahujumu mazungumzo na kanisa.
Wengi sasa wametoa wito wa maandamano kufanyika kumpinga Ezzati.
Chile ni nchi yenye wakatoliki wengi, na ina sheria kali ikiwemo kuharamisha utoaji mimba. Asilimia 52 ya watu nchini Chile wanaunga mkono ndoa za wapenzi wa jinsia moja kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mwaka 2011.
CREDIT: BBC/SWAHILI
Hakuna maoni
Chapisha Maoni