BREEKING NEWS.. JIJI LA DAR KUKOSA MAJI KWA SIKU MBILI MFURULIZO, WAKZI WAAMBIA WACHOTE MAJI YA KUTOSHA LEO.. ZAIDI SOMA HAPA
TAARIFA YA KUKOSEKANA HUDUMA YA MAJI KWA SIKU MBILI JIJINI DAR
Dawasco inawatangazia wakazi wote wa jiji la Dar es salaam na Mji wa Bagamoyo kuwa mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Chini utazimwa kwa wastani wa saa 48 kwa siku za Alhamisi na Iijumaa ya tarehe 30 na 31 Octoba 2014, kuanzia saa kumi na mbili asubuhi, ili kuruhusu mkandarasi (Sino-hydro Corporation ltd) kuunganisha bomba la zamani na bomba jipya (cross-connection) katika mtambo wa Ruvu Chini eneo la Chambezi, Bagamoyo.
Kuzimwa kwa mtambo wa Ruvu Chini kutasababisha maeneo yafuatayo kukosa Maji;
Mji wa Bagamoyo, Mapinga, Bunju, Boko, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi beach na Kawe.
Maeneo mengine ni Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Manzese, Mabibo, Kijitonyama, Kinondoni, Oysterbay, Magomeni, Upanga, Kariakoo, City Centre, Ilala, Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati, Hospitali ya rufaa Muhimbili (MNH), Buguruni, Changombe na Keko.
Wananchi mnashauriwa kuhifadhi maji ya kutosha na kuyatumia kwa matumizi ya lazima.
Au wasiliana na kituo cha huduma kwa wateja namba 022- 2194800
Dawasco inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na ofisi ya uhusiano, Dawasco - Makao Makuu.
Dawasco inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na ofisi ya uhusiano, Dawasco - Makao Makuu.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni