Msemaji wa Wakala wa Huduma za ajira (TaESA) bw. Peter Ugata
(katikati) akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu
mafanikio yaliyofikiwa na wakala huo ikiwemo kuanzisha ofisi za Kanda katika
Mikoa ya Dar es salaam, Dodoma, Mwanza na Arusha ili kusogeza huduma kwa
wananchi. Kulia ni Mratibu wa Huduma za Ajira toka wakala huo Bw. Joseph Haule
na Kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bi Fatma Salum.
Frank Mvungi-Maelezo
Wakala wa huduma za ajira (TaESA) imefanikiwa kuanzisha Ofisi za
Kanda katika Mikoa ya Dar es salaam, Dodoma, Mwanza na Arusha ili kusogeza
huduma zake karibu na wananchi.
Hayo yamesemwa na Msemaji wa wakala wa
Huduma za ajira Bw. Peter
Ugata wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Akifafanua Ugata amesema kuwa wakala imefanikiwa kuanzisha ofisi
katika mikoa hiyo ikiwa ni moja ya hatua za kuboresha huduma zinazotolewa na
wakala huo hapa nchini.
Akieleza zaidi Ugata alisema kuwa wakala huo umeshawahudumia jumla
ya wateja 14,608 kati yao wanaotafuta kazi ni 13,531 waajiri 993 na wakala
binafsi zilikuwa 84.
Kwa upande wa kusajili fursa za kazi Ugata alisema wakala
umesajili fursa za kazi 3,143 kwa kutembelea waajiri 993 katika Mikoa ya
Shinyanga, Kagera, Mara, Mwanza, Singida, Tabora, Iringa, Morogoro, Lindi, Arusha,
Kilimanjaro na Mtwara.
Katika kuboresha huduma zake, Ugata amesema kuwa wakala uko katika
hatua za awali za kuweka mfumo wa kiteknolojia utakaowezesha kukusanya na
kusambaza
taarifa za soko la ajira.
Katika hatua nyingine Ugata amesema wakala kupitia kitengo cha
kuwaunganisha watafutakazi 2,614na waajiri nje ya nchi za nje kama Ujerumani,
Brazil, China, Saudi
Arabia, Denmark, India na Oman.
Katika kuhamasisha wananchi kutumia huduma za wakala huo, Ugata
amesema kuwa wakala umeweka utaratibu madhubuti wa kuratibu na kusimamia
uunganishaji wa watanzania kwenye soko la ajira nje ya nchi ili wapate kazi
zenye staha na kuepukana na biashara haramu ya usafirishaji watu (Human
Traffiking).
|
Hakuna maoni
Chapisha Maoni