Zinazobamba

KILWA ENERGY NA MALIPO YA UKANDAMIZAJI KWA WANANCHI, NI FIDIA YA KUPISHA UJENZI WA NJIA YA UMEME WA KILOVOLT 220 TOKA SOMANGA HADI KINYEREZI, WAITAKA SELIKARI KUINGILIA KATI ZOEZI HILO..

Dar es Saalam. 
Wananchi wa Mji Mpya Majohe, Guluka Kwalala na Ulongoni katika Manispaa ya Ilala  wameiomba Serikali kuingilia kati na kumwamuru mwekezaji wa ujenzi wa njia ya umeme wa  kilovoti 220 kutoka Somanga Mtama  mpaka Kinyerezi, Kilwa Enegy kuwalipa gharama zinazoendana na hali ya maisha ya sasa.
Ombi hilo walilitoa  jana walipokuwa wakijadili kuhusu  dodoso la uhakiki wa mali zao na malipo, walilopewa lilivyokuwa na  upungufu, mapunjo ya mali zao hasa thamani  za nyumba kuwa kidogo  tofauti na gharama  za ujenzi na ununuzi wa kiwanja walizotumia.
Utathmini wa mali na nyumba za wananchi unadaiwa kufanywa na kampuni binafsi iliyofahamika kwa jina la Joransa, ambapo tathmini katika maeneo hayo ilifanyika mwaka 2011 na kutolewa ahadi kuwa malipo ya fidia yangeanza kulipwa baada ya miezi mitatu .
.Baruani Kanoze  akilalamikia kulipwa  fedha kidogo tofauti na thamani ya mali zake, alisema mwekezaji huyo awali aliwahi kusema kuwa atawalipa kwa kiwango kinachoendana na gharama za maisha zilivyo kwa wakati husika jambo ambalo limewashangaza sana. hasa kulingana na kiwango cha malipo kilichotolewa.
‘Ni jambo ambalo haliingii akilini baada ya kuangalia karatasi za tathmini na kukuta gharama zilivyowekwa za viwanja na kupangisha nyumba, kiwanja umewekewa Sh1 milioni na gharama ya kupanga nyumba eti Sh20,000 kwa mwezi, sijui unakwenda kupanga wapi nyumba’ alisema mkazi wa Guluka Kwalala ambaye hakutaka kutajwa gazetini.
 Alisema yeye anamiliki nyumba ya vyumba  vitano, yenye umeme, choo bora pamoja na  kisima cha maji alivyovijenga   kwa zaidi ya Sh40 milioni,  kwenye dodoso la uhakiki wa mali  anaambiwa thamani ya nyumba yake ni Sh6 milioni.
Aidha, walishauri kuliko Serikali kujiingiza katika maafa kwa kukubali mradi huo utekelezwe wakati wananchi hawajaridhika na fidia ao, ni vyema ikafanyika tathmini nyingine ambayo itakuwa ya haki .
Hata hivyo, uongozi wa Kilwa Energy ulipotafutwa kufafanua malipo hayo ya wananchi, simu zao hazikuweza kupatikana.

No comments