Zinazobamba

WAHENGA AJITOSA UNAIBU MEYA DAR

Na Mwandishi Wetu.

Diwani wa kata ya Kinyerezi Manispaa ya Ilala John Ryoba Mrema (WAHENGA) amechukua fomu ya kugombea nafasi ya unaibu Meya katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 21,2025 katika Ofisi za CCM Wilaya ya Ilala Diwani Ryoba amesema kuwa ameamua kuwania nafasi hiyo ili kuwaunganisha madiwani pamoja na kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wasaidizi wake katika kuwaletea wananchi maendeleo.

"Kwanza napenda kuwashukuru wananchi wa kata ya Kinyerezi kwa kujitokeza na kunichagua kwa kura nyingi Oktoba 29 ili niwe diwani wao, pili nimpongeze sana Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuchaguliwa kwa kishindo, pia nampongeza kwa kuunda Serikali ambayo anasaidiwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu Dkt Mwigulu Nchemba pamoja na makamu wa Rais Dkt. Emmanuel Nchimbi."amesema 

Nakuongeza kuwa"Kwenye chama chetu (CCM) kuna utaratibu inapofika wakati wa kutafuta viongozi wa kuongoza halmashauri, utaratibu huo ni kwamba miongoni mwa madiwani  waliochaguliwa kwenye kata na Viti maalumu lazima wapatikane viongozi wawili wa kuendesha baraza la madiwani ambao ni Meya pamoja na Naibu Meya, mimi nimejitokeza kuwania nafasi ya naibu Meya Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam 2025/2030."amesema.

Nakubainisha kwamba "nitaunganisha madiwani, lakini pia nitamsaidia meya atakayechaguliwa na waheshimiwa Madiwani wenzangu ambaye yeye atakua ndiye Mwenyekiti wa vikao vya Halmashauri na mimi nitakua msaidizi wake,

Pili wananchi wote waliotuchagua kutoka kata zote 36 za Wilaya ya Ilala wana matumaini makubwa sana na baraza hili la madiwani la 2025 hadi 2030,hivyo ukipata viongozi wazuri wa kumsaidia Rais, kumsaidia Mkurugenzi, kumsaidia Mkuu wa Mkoa, mimi ninaamini jiji letu la Ilala litapiga hatua kubwa sana kimaendeleo.

Aidha amesema "Ukienda kwenye kata zetu mfano, Kinyerezi, Kitunda, Kimanga,Tabata, wananchi wamekaa wakisubiri sisi tukatekeleze yale tuliyo ahidi na tayari wamekwishaanza kuhesabu itakapofika siku 100 za mheshimiwa Ris na sisi pia madiwani tutaulizwa katika siku hizi 100 mmefanya nini?."amesema Diwani huyo.

Aidha amesema kuwa wananchi wanataka mahitaji mbalimbali ikiwemo maji, miundombinu ya barabara, mikopo, hivyo basi kwa dhamira yake ya dhati amesukumwa  kuchukua fomu  ili agombee unaibu Meya. 

No comments