RAIS SAMIA:TUTAONGEZA UZALISHAJI WA UMEME KUFIKIA MEGAWATI 8000 IFIKAPO 2030

📌Mikoa yote nchi nzima kuungwa kwenye Gridi ya Taifa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa Serikali imejiwekea malengo ya kuongeza uzalishaji wa umeme maradufu hadi kufikia megawati 8,000 ifikapo mwaka 2030, ili kuendana na kasi ya ukuaji wa uchumi na mahitaji ya nishati ya umeme nchini.
Akilihutubia Bunge jijini Dodoma tarehe 14 Novemba 2025 wakati akilifungua Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Samia amesema katika kipindi kilichopita, Serikali imefanikiwa kuongeza uzalishaji wa umeme kutoka megawati 1,600 hadi zaidi ya megawati 4,000, hatua iliyowezesha vijiji vyote nchini kufikiwa na miundombinu ya umeme.
“Tunapoelekea mwaka 2030, tumejiwekea lengo la kuongeza uzalishaji wa umeme maradufu na kupanua mtandao wa umeme ili kufikia vitongoji vyote nchini.”Amesema Rais Samia.
Amebainisha kuwa Tanzania imebarikiwa kuwa na vyanzo nyingi za nishati ikiwemo maji, jua
No comments
Post a Comment