SERIKALI YA AAFP KUWATAFUTIA MASOKO YA UHAKIKA WAKULIMA.
Katibu Mkuu AAFP Taifa Rashid Rai
Na Mwandishi Wetu.Matombo Morogoro.
Chama Cha AAFP kimesema kuwa endapo kitashika dola kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29 Mwaka huu kitahakikisha kinateua Waziri wa Kilimo ambaye atakua na kazi maalumu ya kupigania haki na kuifanya kazi ya Wakulima kuheshimika.
Hayo yamesemwa Septemba 2,2025 na Katibu Mkuu wa Chama hicho Rashid Rai wakati akimnadi Mgombea urais kupitia Chama hicho Kunje Ngombale Mwiru pamoja na mgombea mwenza Chumu Abdallah Juma katika kata ya Matombo Jimbo la Morogoro Kusini.
Mgombea Urais wa JMT Kinje Ngombale Mwiru(kuria) kushoto kwake ni Mgombea mwezi Bi.Chumu Abdallah Juma,wakiwa kwenye kampeni kata ya Matombo Jimbo la Morogoro Kusini.
"Kazi ya Serikali ya AAFP kupitia Waziri anaehusika na mambo ya Kilimo unapofika msimu wa Kilimo ataenda kutafuta masoko,katika masoko ya Kimataifa huko Ulaya,Amerika na Asia kwa ajili ya kujua kwamba katika msimu wa Kilimo wa 2024/2025 soko la dunia linataka mazao gani kutoka nchi za Afrika kabla ya Wananchi hawajaanza shughuli za Kilimo."amesema Rai
Baadhi ya Wananchi wa Matombo wakisikiliza Sera za AAFP.
"Nakuongeza kuwa Waziri aje aseme kwamba nimekwenda soko la dunia India wanataka Mbaazi,China wanataka ufuta,Canada wanataka Pamba,Marekani wanataka Mkonge,kwahiyo nimepata oda ya mazao haya tani kadhaa,msimu wa Kilimo wa Mwaka huu 2025/2026 limeni Ufuta,Pamba,Kahawa, kwasababu Masoko yake yapo."
Aidha amesema hatua hiyo itasaidia mkulima wakati analima awe na uhakika analima zao la biashara ambalo lina uhakika wa kuuzwa,ilivyo sasa mkulima anabahatisha,ile hali ya kubahatisha kufanya Kilimo cha bure bila soko la uhakika,hali hii itaondoka pale tu Wananchi watakapo kichagua chama cha wakulima AAFP kushika dola.
Baadhi ya Wananchi wa Matombo wakisikiliza Sera za AAFP.
No comments
Post a Comment