Zinazobamba

AAFP KUIPELEKA CCM MAHAKAMA YA KIMATIFA



Na Mwandishi wetu Pwani.
*Nikutokana na kuandaa mkusanyiko mkubwa wa kampeni bila kuweka vyoo.
"Mwiru aahapa kufanya hivo baada tu ya kuapishwa kua rais Oktoba 29.mwaka huu.
Na Mwandishi Wetu.Malandizi Pwani.

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Wakulima (AAFP)Kunje Ngombale Mwiru amesema atakipeleka Mahakama ya Kimataifa Chama Cha Mapinduzi kutokana na  kukusanya halaiki ya watu huku kukiwa hakuna miundombinu ya vyoo kwa ajili ya kujisadia.

Mheshimiwa Mwiru amesema hayo leo Septemba 9,2025 Mlandizi Wilaya ya Kibaha Vijijini,Jimbo la Kibaha Vijijini Mkoani Pwani wakati akianza ziara ya kampeni za uchaguzi mkuu Mkoani humo,nakuoneshwa hali ya kuchukizwa na tabia ya CCM ya kukusanya watu kwenye kampeni zake huku hakuna vyoo vya kujisaidia Wananchi hao.

"Nikingia madarakani tarehe 29,chama tawala nakipeleka mahakamani,tena nakipeleka mahakama ya Kimataifa, wenzetu(CCM)wanachokifanya wanawasomba watu kutoka Wilaya mbalimbali pale mahali wanapowapeleka hakuna Mazingira yakinifu ya huyu bianadamu kupata huduma pale,wanawajaza hata huduma ya vyoo hamna" amesema.

Kuhusu ahadi ya kutatua changamoto za wananchi wa Wilaya ya Kibaha Vijijini mheshimiwa Mwiru anasema kuwa zinatokana na kukosekana kwa uzalendo hivyo atahakikisha Watanzania wanafundishwa uzalendo kwani ndio kipaumbele chake cha kwanza.

 "Ndugu zangu Watanzania,hizi changamoto zote tunazoziona ni kwasababu ya watu kukosa uzalendo,na ndio maana Serikali yangu ya mchakamchaka nimepanga tarehe 29 nikiapishwa nitaweka madawati ya Wazee waliostaafu kwenye Serikali ili waendelee kuwafundisha Watanzania uzalendo na maadili.

Nakuongeza"Ndugu zangu wana Mlandizi hapa kuna changamoto nyingi,kuna barabara ya kutoka Bagamoyo,hii barabara imeshatathiminiwa muda mrefu,watu wake hawalipwi fididia,nina imani nikingia madarakani nitakachokifanya vikao vyote vya Halmashauri wanavyokaa madiwani,nilazima nitaweka idara ya usalama kusimamia ahadi zao na mapato yote ya ndani katika halmashauri zote.
*Foleni Dar es salaam - Morogoro 

Kwasababu vyanzo vingi tunavyo vya kutengeneza barabara nitajenga barabara maalumu kutoka Dar es salaam kuelekea Arusha,barabara hiyo itatenga barabara nyingine ya pili ambayo ikifika Msamvu Morogoro inaelekea Makao Makuu ya nchi Dodoma,nitajenga barabara nyingine ya tatu yenyewe ni maalumu kwa ajili ya magari yanayoelekea barabara ya Iringa ili kukuza mawasiliano na uchumi wa Taifa.

*Vijana kuanzia miaka 18 kupewa power tiller.

"Hapa Mlandizi kuna Kilimo kinaendelea ,kama inavyosemwa siku zote ,kijana wa aina yeyote kuanzia umri wa miaka 18 ni lazima atakabidhiwa power tiller kwa ajili ya Kilimo, power tiller hiyo haitakuwa na deni lolote,mimi kama Serikali nitwajibika ,Mtanzania anataka maendeleo aishi kama wanavyoishi watu ulaya,leo hii wanaishi kwa shida kutokana na mikopo ya utumwa."amesema Mheshimiwa Mwiru.
*Mikopo bila riba kwa akina mama wajasiriamali.

Aidha amesema kuwa wakina mama wamekua wakikimbia familia zao kutokana na kushawishiwa na watu kupewa mikopo badala yake wanakua kama watumwa wa kukimbiakimbia hovyo,hivyo Serikali yake haitokubaliana na hali hiyo,na wakina mama wote watapata mikopo bila riba ndani ya miaka mitano ya urais wake.

*Mafisadi kutafunwa na mamba Ikulu.

Aidha amesisitiza kuwa Serikali yake itaendelea kupambana na Mafisadi,nakusema kuwa atakua rais wa mfano Afrika ambapo atatoa miezi miwili kwa idara ya usalama kwa ajili ya kuchimba bwawa la mamba Ikulu kwa ajili ya kuwashughulikia Mafisadi hao.

"Taifa hili linahitaji maheshimiano,watu wamechoka kuheshimiana,mtu anakula pesa anatembea na tumbo lake mitaani,mimi nitakunja kiti nita ahirisha ziara yangu ya urais nitasubiri siku maalumu ya mafisadi watakaoingia Ikulu kwangu ili wapambane na mamba,"amesema
*Madereva Bodaboda kupewa pikipiki za mkopo.

Aidha amesema kuwa bodaboda wamekua wakipata changamoto ya mkataba kutoka kwa waajili wao,hivyo amewahakikishia kuwapatia pikipiki ambazo sio za mkataba,bali watafanya kazi na kurejesha pesa za mkopo wa pikipiki pekee,na endapo akimaliza marejesho basi pikipiki hiyo itakua mali yake.

*Matibabu bila malipo.

Serikali yake hakutakua na huduma ya  bima ya Afya,ambapo Mtanzania yeyote akizaliwa atatibiwa bure kwa  miaka yote ya uhai wake  hadi mauti itakapomkuta,nakwamba bima zitakua kwenye vyombo vya usafiri  pekee.

*Maiti Kudaiwa.

Aidha amesema kuwa daktari wa aina yeyote atakae zuia maiti katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwenye jeneza daktari ataenda mwenyewe.

"Fisadi anadaiwa bilioni mbili lakini unakaa nae kitako kujadili namna ya kuzilipa fedha hizo,halafu maiti inazuiliwa eti inadaiwa,weeee Serikali yangu watakiona cha moto"amesema 
*Walimu kuishi kifalme.

Amesema kuwa walimu wanaishi kwa shida,mishahara duni,ambapo Mwalimu huyo ndie aliyemfundisha fisadi,hivyo Serikali yake walimu wote wataishi kifalme kwa kupata mishahara mikubwa na makazi bora.

*Askari polisi kupata mshahara mnono.

Ameendelea kuahidi kuwa askari polisi watapata mishahara minono kutokana na kazi kubwa ya kizalendo wanayoifanya usiku na mchana.

*Mabomba ya umeme kupita chini ya ardhi.

Aidha amesema kuwa Watanzania wamekua na asilimia ndogo ya kuishi kutokana na athari ya umeme kwasababu ya nyaya za umeme kupita juu ya nguzo,endapo upepo au kibunga kikitokea umeme unakatika,katika nchi za ulaya hali hiyo haipo,hivyo Serikali yake ya mchakamchaka itahakikisha nyaya zote za umeme zinapita chini ya ardhi kwa kutumia mabomba. 

*Miundombinu ya barabara.
Nitaweka mashine za kuponda mawe na kusaga kokoto" Crusher"ili tujenge barabara za zege,tuachane na mambo ya lami ambayo ni mpango wa watu wachache ambao wanapiga fedha za miradi 
*Maji.
Aidha amesema ndani ya mwaka mmoja akiwa  madarakani hataki  kuona nyumba yoyote Wilaya ya Kibaha Vijijini inakosa Maji safi na salama.

*Wazee kupata kima cha chini cha mshahara.

Aidha amesema kuwa Wazee wote watapata kima cha chini cha mshahara ili waweze kujikimu kimaisha.

*Amesisitiza amani kwa Taifa.

Mgombea huyo wa urais kupitia Chama Cha Wakulima (AAFP)amesema kuwa amani ndio silaha ya mafanikio yote duniani,viongozi wanatakiwa waasisi wa amani hiyo akitolea mfano hayati Mwalimu Nyerere na Karume ambao ambao walisimamia Vyema misingi ya amani. 

No comments