MAFUNZO YA TUMIA ULICHONACHO KUPATA USICHOKUWA NACHO KUTOKA TGNP YAIFIKIA KATA YA MSONGOLA
Afisa mtendaji wa kata ya Msongola Renatus Luhungu amelipongeza shirika la TGNP kwa kuwapa elimu baadhi ya wakazi wa kata hiyo juu ya kujiletea maendeleo kwa rasilimali walizonazo na siyo kuitegemea serikali kwenye kila kitu.
![]() |
Afisa mtendaji wa kata ya Msongola Renatus Luhungu akipokea risala kutoka kwa mmoja wa muhitimu wa mafunzo ya kutumia ulichonacho ili kupata usichokuwa nacho yanayoendeshwa na Taasisi ya TGNP. |
Akitoa pongezi hizo mapema jana April 30, 2025 katika ofisi ya kata ya Msongola ambapo wahitimu 25 wa mafunzo hayo waliweza kutoa mrejesho kwa viongozi wao ngazi za Mitaa na kata, juu ya kile walichofundishwa kwa siku tano mfululizo na maafisa wa TGNP.
Amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu na yatasaidia kuweza kuwaamsha wanachi kujitokeza kuweka nguvu kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo na pia kuwa na uchungu kwa kuwa na wao ni sehemu ya hiyo miradi.
Ameongeza kuwa kwenye suala la ukatili wa kijinsia kwenye kata ya Msongola kwa sasa matukio yamepungua na hii ni kutokana kuwepo na Club mashuleni lakini pia ushirikiano mzuri uliyopo baina ya Polisi dawati pamoja na viongozi wa kata.
Kwa upande wake mshiriki wa mafunzo Anjera Zacharia amesema kuwa alichokipenda katika mfunzo hayo ni dhana ya kutumia ulichonacho ili kupata usichokuwa nacho, na kusema kuwa changamoto nyingi zimekuwa zikielekezwa kwa serikali, lakini baada ya mafunzo haya jamii itaweza kubadilika na kwa sasa tutachukua hatua wenyewe kabla ya mamlaka kufika.
Na kuongeza kuwa "baada ya mafunzo tutakwenda kuleta vuvuga la pamoja katika mitaa yetu tushirikiana na wanachi wenzetu kuhakikisha changamoto zilizo ndani ya uwezo wetu tunakabiliana nazo na siyo mpaka kusubiri serikali ije kutaua mfano. kusaidi kwa rasilimali nguvu kwenye ujenzi wa huduma za kijamii kama Shule, Zahanati, Vivuko nk.
Naye muwakilishi wa TGNP Malta Kikwa amesema kuwa huu ni mradi uliyopo katika halmashauri za Dar es salaam pamoja na halmashauri ya Kishapu mkoa wa Shinyanga na wenye lengo la kuhamasisha wananchi waweze kuanzisha na kusaidia uendelezaji wa miradi mbalimbali katika maeneo yao.
Amemalizia kwa kusema kuwa mradi huu unatambulika kwa jina la "Engage" na unasimamiwa na TGNP chini ya ufadhiliwa na Taasisi ya COADY yenye makao makuu yake nchini Canada.
![]() |
Anjera Zacharia Mshiriki wa mafunzo ya kutumia ulichonacho ili kupata usichokuwa nacho yanayoendeshwa na Taasisi ya TGNP akitoa ufafanuzi wa jambo mbele ya Viongozi wa Kata ya Masongola . |
![]() |
Baadhi ya Viongozi wa Kata ya Msongola wakifuatilia matukio katika mrejesho uliyofanywa na wahitimu wa mafunzo ya kutumia ulichonacho ili kupata usichokuwa nacho kwa viongozi wao wa kata. |
Wahitimu mafunzo ya kutumia ulichonacho ili kupata usichokuwa nacho yanayoendeshwa na Taasisi ya TGNP wakionyesha igizo mbele ya Viongozi wa kata ya Msongola. |
![]() |
Afisa mtendaji wa kata ya Msongola Renatus Luhungu akiongea na washiriki wa mafunzo ya kutumia ulichonacho ili kupata usichokuwa nacho yanayoendeshwa na Taasisi ya TGNP. |
![]() |
Washiriki wa Mafunzo wakifuatilia maelekezo ya Viongozi wao pamoja na wakufunzi kutoka TGNP, jinsi ya kufanya kazi na Jamii yao ili kuweza kuleta maendeleo katika maeneo wanayoishi. |
![]() |
Picha ya Pamoja kati ya wahitimu pamoja na Waraghibishi kutoka shirika la TGNP. |
No comments
Post a Comment