Dkt. Faustine Ndugulile
NA Mussa Augustine
Serikali ya Tanzania
imemtambulisha Dkt. Faustine Ndugulile kuwa mgombea wa nafasi ya Mkurugenzi wa
Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa ukanda wa Afrika katika awamu nyingine ya
miaka kumi.
Hayo yalisemwa Mei 8,2024
jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Mh.Januari Makamba wakati wa hafla ya utambulisho huo iliyohudhuriwa
mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali nchini, ambapo amempongeza Dkt.
Ndugulile kwa kuidhinishwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwania nafasi hiyo
itakayoleta heshima kwa Tanzania.
Waziri Makamba amesema
kuwa kutambulishwa kwa Dkt. Ndugulile ni ishara ya kufungua milango ya kampeni
kuelekea kuwania nafasi hiyo muhimu inayobeba maslahi ya wananchi katika
masuala mazima ya afya zao.
"Dkt. Ndugulile ni
mtu ambaye nimemfahamu kwa muda mrefu, ni mchapa kazi ambaye amebobea katika
masuala ya afya, akihudumu katika nafasi mbalimbali Serikalini ikwemo Waziri wa
Afya, na amefanya kazi na taasisi mbalimbali za kimataifa, hivyo ninaimani
anafaa kuwa katika nafasi hiyo," amesema.
Aidha meeleza kuwa hadi
sasa wakati kampeni ya Dkt. Ndugulile
ikizinduliwa ni kwamba ameshapata uungwaji mkono wa Jumuiya ya Nchi za Kusini
mwa Afrika (SADC).
Nakuongeza kuwa” Uchaguzi utafanyika Mwezi wa
nane Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,hivyo tuna matumaini Makubwa
Mgombea wetu wa mara ya kwanza kutoka nchini Tanzania atashinda katika kinyang’anyiro
hicho.
Nae Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema ni mara
ya kwanza kwa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla kutoa mwakilishi wa
kugombea nafasi ya Mkurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika.
"Mgombea wetu anauzoefu mkubwa katika
masuala ya afya Duniani, hivyo hii ni nafasi sahihi kwa Dkt. Ndugulile,hivyo kutokana
na ujuzi alionao Dkt. Ndugulile katika masuala ya Afya, anaamini atapeleka
uzoefu mzuri WHO hususan katika utungaji na uboreshaji wa Sera za Afya kwenye
Shirika hilo.”amesema Waziri Ummy.
Naye Dkt. Faustine Ndugulile ambaye nimgombea
wa nafasi hiyo amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumpa kibali na kumuunga
mkono katika kuwania nafasi hiyo.
Dkt.Ndugulile amesema kuwa WHO kwa Kanda ya
Afrika inasimamia nchi takribani 48, hivyo amesema kuwa miongoni mwa mambo
atafanya akipata nafasi hiyo ni pamoja na kuendeleza mabadiliko katika shirika.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni