Zinazobamba

MBUNGE WA JIMBO LA EMBAKASI MASHARIKI BABU OWINO AWAFUNDA VIJANA WA ACT-WAZALENDO.


Vijana wametakiwa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu ujao ili kupigania wananchi Katika nyanja mbalimbali za maendeleo ambazo Watanzania wanataka.

Wito huo umetolewa leo februari 29,2024 na Mbunge wa jimbo la Embakasi Mashariki Kutoka Kenya Paul Owino Maarufu kama Babu Owino wakati akifungua Mkutano Mkuu ngome ya vijana ACT-Wazalendo ukiwa na lengo la kufanyauchaguzi wa kupa viongozi wa Kitaifa wa ngome hiyo ambapo amesema vijana ni viongozi wa leo,kesho na kesho kutwa na wasiendekeze msemo usemao vijana ni viongozi wa kesho.

Ameongeza kuwa Vijana wanatakiwa kutambua kuwa Uongozi sio vyeo,bali ni jukumu la kufanya mabadiliko kujenga nchi na Mamlaka sio kutumia kibinafsi bali kutumikia watu, kiongozi bora ni yule anayejitolea kwa ustawi watu wake anaye elewa mahitaji ya watu wake na pia anaye wajibika kwa matendo yake.

"Kijana ukitka kitu pigania ukingoja kupewa hutapewa,kama huwezi kupewa chukua" 

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo Ado Shaibu amesema chama kinawategemea sana vijana hakiwezi kutekeleza mambo yake bila kuwa na vijana,tunagemea vijana hao wawe na weredi mkubwa.

"Leo ni siku ya kuamua kuwa na viongozi wa ngome watakao wajibika kujenga chama,leo ni siku ya kuamua kuchagua viongozi watakao wajibika kupigania maslai ya vijana na taifa kwa ujumla"

"Tunawaamini wapiga kura watatuletea viongozi watako tumikia chama kwa miaka mitano ambao watakuwa ni chachu ya maendeleo,"Tuchague mmoja,tubaki woja kwasababu sote ni washindi".

Kwa upande wake Mwenyekiti wa ngome ya vijana ACT-Wazalendo Abdul Nondo amesema leo ni siku adhimu ambayo imejumisha viongozi na wajumbe wa Halmashauri kuu ngome ya vijana mikoa yote tanzania na kuweza kisaidia chama kupata viongozi.

Amewasisitiza viongozi katika matawi,mashina na kata,jimbo kuhakikisha wanapigania maslai ya chama na jamii inayomzunguka kuhakikisha wanasemewa changamoto zao.


katibu mkuu ngome ya vijana Mwanaisha mndeme amesema Kwa mara ya kwanza wameweza kutimiza lengo la uchaguzi kuanzia ngazi ya matawi,wilaya na taifa ,kichama wana mikoa 28 huku Zanzibar wakiwa ni 11 na kufanya kuwa na jumla ya mikoa 39. Pia Akidi ilitimia kwa kiwa na jumla ya watu122 sawa na asilimia 85.3 kati ya wajumbe 143.


Hata hivyo Mwakilishi wa Ngome ya vijana chadema Twaha Mwaipaya amewataka wajumbe hao kuchagua viongozi walioimara watakaoweza kupigania maslai ya vijana na taifa kwa ujumla.ambai pia watakaoweza kuwaungamisha vijana wa taifa zima bila kuja itikadi zao wala vyama.


Hakuna maoni