Zinazobamba

Waziri Mkuu Majaliwa Atoa neno katika ufunguzi waTamasha la Utamaduni Mkoani Dar es salaam

Na Mussa Augustine.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ameziagiza halmashauri za Wilaya pamoja  na Mikoa yote nchini kuwawezesha Watoto kujifunza mila zao za asili ili kuwafanya watambue historia wakiwa bado wana umri mdogo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa.
Ametoa agizo hilo Jana kwenye ufunguzi wa Tamasha la Kwanza Kitaifa la utamaduni linalofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini dar es salaam ambapo lina ujumbe usemao "Utamaduni Wetu,Fahari yetu,Tujiandae kuhesabiwa na kazi iendelee"

Aidhama Waziri Mkuu Majaliwa amesema kwamba muasisi wa Taifa  hili Hayati Mwalimu Julius  Nyerere alisema kwamba  Utamaduni ni roho na kiini Cha Taifa hivyo lazima kuendelea kuuthamini na kuuendeleza ili Taifa liheshimike.

" Naiagiza Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo kushirikiana wadau mbalimbali ambao wanandaa matasha haya pia wazazi wanaposikia matamasha haya wawapeleke Watoto kujifunza wao kujifunza mila zao za asili kwani itasaidia Watoto kufahamu historia za mkoa wanapoishi" amesema Kassim Majaliwa.

Awali Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Mohamed Mchengerwa amesema kwamba Tamasha la Utamaduni lina lengo kubwa la kuamsha ari ya kujali na kuthamini Utamaduni wa  Watanzania na kuachana na tamaduni za kigeni ambazo zinapoteza asilia ya mtanzania.

" "Siku za nyuma tumesahau Utamaduni wetu nakujali tamaduni za magharibi ,rais wetu mpendwa Mama Samia Suluhu Hassani ametaka tufanye matamasha haya ili kumuenzi mtanzania na Utamaduni wake,utamaduni ndio maisha yetu,Taifa lolote lisilo na Utamaduni ni Taifa ambalo ni mateka au Taifa mfu" amesisitiza Waziri Mchengerwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa (katikati) wakifurahia ngoma wakati Waziri Mkuu alipofungua Tamasha la Kwanza la Utamaduni kwenye Uwanja wa Uhuru, Temeke Mkoani Dar es salaam, Julai 2, 2022.  Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya  Utamaduni, Sanaa na Michewzo, Dkt. Hassan Abbas. 
Nae Katibu tawala Mkoa wa Dar es Salaam Hassan Lugwa ameahidi kuhakikisha Ulinzi na Usalama utaimarishwa ili kulifanya Taifa Hilo kufanikiwa nakwamba ofisi ya Mkoa wa Dar es salaam imeshirikishwa ipasavyo katika uandaaji wa Tamasha hilo.

Hiyo ni mara ya kwanza kwa tamasha hilo la Utamaduni kufanyika nchini ambapo kilele Cha Tamasha hilo linaloenda sambamba  na siku ya Kiswahili duniani linatarajiwa kuadhimishwa mwishoni mwa wiki ijayo ambapo Kitaifa litafanyika jijini Dar es salaam ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan.
Baadhi ya washiriki wa Tamasha la Utamaduni wakifuatilia matukio mbalimbali katika Tamasha hilo mapema Jana mkoani Dar es salaam.

No comments