NSSF yazindua Mfumo Mpya Wa Ukusanyaji Mapato Daraja la Nyerere.
Na Mussa Augustine.
Serikali kupitia Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) imezindua Mfumo mpya ambao utasaidia kulipia gharama za magari yanayopita daraja la Nyerere lililopo Kigamboni kwa njia ya vifurushi vya bei nafuu ikiwemo kifurushi cha saa 24 , siku saba, pamoja na mwezi.
![]() |
| Meneja Uwekezaji wa NSSF Bw. Victor Luvena akizungumza na Waandishi wa habari kwenye daraja la Nyerere Kigamboni. |
Akizungumza leo na Waandishi wa habari wakati wa ziara ya kutembelea Daraja hilo pamoja na mradi wa ujenzi wa nyumba wa Dungu Project Kigamboni inayotekelezwa na NSSF, Meneja Uwekezaji wa Mfuko huo Bw.Victor Luvena amesema mfumo huo unakwenda kutatua kero na kuleta ahueni kwa wananchi wanaotumia daraja hilo .
"Mfumo huu unaenda kurahisisha ulipaji wa tozo za daraja kwani awali watumiaji wa daraja hili walikua wanatumia muda mwingi yaani dakika hadi 10 ,lakini kwasasa wanatumia sekunde tu kulipia ,na gharama zake ni ndogo sana ukilinganisha nazile za awali" amesema Bw.Luvena.
![]() |
| Msimamizi daraja la Nyerere Bw. Emmanuel Masika akitolea ufafanuzi namna ya ulipaji wa tozo kupitia mfumo mpya wa vifirushi uliozinduliwa na NSSF. |
Kwa upande wake Msimamizi wa Daraja la Nyerere Kigamboni Bw. Emmanuel Masika amesema kwamba watumiaji wa daraja hilo watalipia kifurishi cha siku kwa shilingi 2500, kifurushi cha wiki 12000 huku cha mwezi kikiwa ni shilingi 35000 ambapo amesisitiza kuwa punguzo ya gharama hizo imeleta ahueni kwa watumiaji wa darajal la Nyerere.
Sambamba na ziara hiyo imetembelea mradi nyumba wa Dungu,nakutoa wito kwa Wananchi kuchangamkia fursa ya kupata Makazi ya kudumu kupitia mradi wa nyumba ambazo zimejengwa na Mfuko huo kwa ajili ya kupangisha na kuwauzia watu wanaohitaji kwa gharama nafuu huku wakilipia kidogokidogo ndani ya miaka 15.
Meneja umiliki wa NSSF Bw.Geoffrey Thimoth amesema kwamba mfuko huo umefanikiwa kujenga nyumba za gharama tofauti ambazo ni nyumba za kuanzia kiasi cha shilingi milioni 131, milioni 148, milioni 192, milioni 236 pamoja na milioni 497 ambapo mteja analipa asilimia 10 ya gharama ya nyumba anayoitaka halafu kiasi kingine analipa kidogokidogo kwa Muda wa miaka kumi na tano.
" Sisi kama NSSF jukumu letu la msingi kulipa mafao,na mafao hayo yatumike pia kujenga nyumba zakuzipangisha au kuziuza kwa bei nafuu ,hivyo tuna miradi mikubwa mitatu ambapo hapa tulipo ni mradi unaojulikana kama Dungu project wenye uniti mia nane za nyumba,lakini pia tuna mradi mwingine Kijichi na Tuangoma" amesema Bw.Thimoth.
![]() |
| Mchekeshaji Steve Nyerere akizungumzia na Waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa ziara ya kutembelea Daraja la Nyerere na mradi wa Nyumba wa Dungu Kigamboni. |
Kwa upande wao Mabalozi wa NSSF akiwemo Msanii wa vichekesho Steven Mengele "Steve Nyerere",Msanii wa Bongo fleva Willium Lymo maarufu kama "Bill Nass" pamoja Mussa Hussein wamesema Kwa nyakati tofauti wamewaasa wasanii na wananchi Kwa ujumla ambao Wana malengo ya kumiliki nyumba kuchangamkia fursa hiyo,ili kuiandaa kesho yao.



No comments
Post a Comment