Tanzania Kuazimisha Tamasha la Kwanza la Kitaifa Kuhusu Utamaduni
Na Mussa Augustine.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Tamasha kubwa la Kwanza Kitaifa la Utamaduni na Siku ya Kiswahili Duniani litakalofanyika Kuanzia Julai Mosi Mwaka huu jijini Dar es salaam lenye ujumbe usema" Utamaduni Wetu;Fahari yetu;tujiandae kuhesabiwa ,Kazi iendelee"
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mkuu wa Mkoa huo Amos Makala amesema kwamba Tamasha hilo litafanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia Julai 1 hadi Julai 3 Mwaka huu ikiwa lengo ni kuifanya jamii kutambua,kuthamini na kuendeleza urithi na Utamaduni waliorithi kutoka kwa wazazi na kuenzi lugha ya kiswahili
"Kuandaliwa Kwa Tamasha hilo ni utekelezwaji wa maagizo ya Mheshimiwa rais Samia Suluhu Hassani aliyoitoa Mkoani Mwanza Septemba 8 Mwaka 2021 katika Tamasha la Utamaduni Mwanza ambapo aliagiza matamasha yafanyike Kwa mzunguko kila Mkoa na washindi wapatiwe tuzo" amesema RC Makalla.
Naomba ninukuu agizo la Mh. Raisi " Matamasha haya yafanyike kwa mzunguko kila Mkoa ili Watanzania waweze kujua mila na desturi zetu za kila Mkoa na kila pembe ya Tanzania ,pia kuandaa mashindano yatakayoshindaniwa na Mikoa yote ambapo mshindi atapata Tuzo,mwisho wa kunukuu" ameongeza.
Hali kadhalika amendelea kufafanua kuwa kutakuwa na matukio mbalimbali yatakayohusishwa kwenye tamasha hilo ambapo Julai 1-3 Usiku wa taarabu katika fukwe za coco(Coco Beach) ikihusisha wasanii nguli akiwemo Khadija Kopa, Isha Mashauzi,Patricia Hilary pamoja na vikundi kutoka Safina Modern Taraabu,First Class,Nakshi Nakshi pamoja Vikundi kutoka nje ya Nchi za Burundi,Kenya,na Visiwa vya Comoro.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es salaam amesema kwamba baada ya Julai 4 kutakuwa na maandamano ya amani kutoka Wilayani Temeke hadi uwanja wa Uhuru jijini hapa,nakwamba yatahusu lugha ya kiswahili na utoaji wa haki na yataongozwa na Waziri wa katiba na Sheria Dkt Damasi Ndumbaro.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Maendeleo ya Lugha kutoka Wizara ya Sanaa Utamaduni na Michezo Dkt Mnata Resani amesema kuwa Julai 6 kutakuwa na kongamano linalohusu mchango wa kugha ya Kiswahili katika harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika na mchokoza mada katika kongamano hilo ni Balozi Mstaafu Ame Mpungwe pamoja na viongozi kutoka nje ya Nchi.
"Kama mnavyofahamu UNESCO imeipa lugha ya kiswahili heshima kwa kuipa siku yake ya kuiadhimisha ambayo ni Julai 7 kila Mwaka, hivyo Tanzania ambayo ndiyo yenye Johari hii kiswahili imeandaa Maadhimisho ya siku ya kiswahili Duniani (MASIKIDU) itaadhimishwa mara ya kwanza Duniani"amesema Dkt Resani
Aidha ameongeza kuwa Julai 7 mwaka huu Kwa mara ya kwanza ni maadhimisho ya siku ya kiswahili duniani ,huku kitaifa tukio linatarajiwa kufanyika katika Viwanja vya Uhuru jijini Dar es salaam ,nakwamba mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassani
"Kiswahili ni lugha pendwa na imekuwa ikizidi kuenea Duniani kote hivyo baraza la kiswahili limekuwa na utaratibu wa kuwatambua wataalamu wa lugha hiyo Kwa kuanzisha kanzi data ili wajisajili lengo ni kujua takwimu yao" amesisitiza Dkt Resani.
Hata hivyo ametumia fursa hiyo kutoa with kwa Wananchi kushiriki katika matukio hayo ya kihistoria ,ambapo pia wageni kutoka nje ya nchi ya Tanzania watakuwepo kuja kuunga mkono siku ya kiswahili duniani ,nakwamba marais wastaafu Joachim Chisano kutoka Msumbiji pamoja na Sam Nujoma kutoka Namibia watahudhulia katika maadhimisho hayo.

No comments
Post a Comment