Diwani Bagamoyo atembea kwa miguu kusikiliza kero za wananchi
![]() |
| Diwani wa Kata ya Nianjema iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Mhe.Abdul Pyalla wa Kati kati aliyevaa kofia akizungumza na wananchi wakati wa ziara yake ya kikazi. |
Mwandishi wetu
Diwani wa Kata ya Nianjema Mh. Abdul Pyalla amefanya
ziara ya mtaa kwa mtaa lengo likiwa kusikililiza kero na changamoto zinazowakabili
wananchi na kuzipatia ufumbuzi.
Akizungumza na baadhi ya wananchi katika mtaa
wa Magomeni A pamoja mtaa wa Nianjema B, Mh. Abdul Pyalla alisema kwamba
ameamua kuwatembelea wananchi ili kuweza kusikililiza kero zao mbali mbali na
kuweza kuzitafutia ufumbuzi.
Pia alisema kuwa katika ziara hiyo amejipanga
vilivyo kutokana na kuambatana na wataalamu mbali mbali kutoka taasisi za
serikali pamoja na mashirika ya umma nia na madhumuni ni kupata majibu ya kina
kutoka kwa wataalamu husika.
“Ziara yangu hii lengo lake kubwa ni kutembelea
mitaa mbali mbali ambayo ipo katika kata yangu ya Nianjema na dhumuni lake
kubwa ni kusililiza kero na changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi
wangu katika sekta tofauti,”alisema Diwani huyo.
Aidha aliongeza kuwa lengo lake kubwa ni
kuhakikisha kwamba anaweka mipango madhubuti kwa kushirikiana na viongozi
wenzake pamoja na taasisi za kiserikali kwa kuwaletea huduma mbali mbali za
kijamii ikiwemo upatikani wa umeme, maji, afya, elimu pamoja na mahitaji
mengine.
“Nashukuru pia katika mkutano huu tumeshirikiana
kwa ukaribu na taasisi tofauti Kama vile Tanesco, Dawasa, Tarura, TFS, pamoja
na wenzetu wa benki ya NMB ambao wameweza kutoa fursa ya utoaji wa elimu mbali
mbali na umuhimu wa kujiunga na bima kupitia benki hiyo,” alisema
Katika hatua nyingine aliahidi kuendelea
kushirikiana bega kwa bega na taasisi zote za kiserikali pamoja na mashirika ya
umma kwa lengo la kuweza kutatua changamoto za wananchi na kuweka mipango ya
pamoja katika kuwaletea maendeleo yenye tija kwa wote.


No comments
Post a Comment