Masheikh, Maimam kuburuzwa mahakamani
SHEKHE wa Mkoa wa Dodoma (BAKWATA) Mustaph Rajabu amesema mashekhe, maimamu na walimu ambao watakaongundulika kufungisha ndoa kwa kutumia vyeti feki wataburuzwa kwenye vyombo vya kisheria ikiwemo na kuwaondoa kwenye nafasi zao za madarakani.
Aidha Shekhe Mustapha, amesema kuwa mashehe,maimamu na walimu
ngazi ya kata ambao wanaoshindwa kujitambua kwenye kazi yao watalazimika
kupisha kwenye nafasi zao
Shekh Rajabu ametoa onyo hilo alipokuwa akizungumza na viongozi
hao wa ngazi mbalimbali wakiwemo mashekhee,maimamu na walimu kwenye semina ya
kuwajengea uwezo iliyofanyika jijini Dodoma.
Alisema kuna baadhi ya walimu maimamu ambao siyo waaminifu kwenye
nafasi zao kutokana na kujiingiza kwenye utapeli wa kuwafungisha wanandoa kwa
kutumia vyeti visivyotambuliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).
“Mimi kama kiongozi wenu wa
mkoa kwa kushirikiana na wasaidizi wangu wa wilaya,kata.mitaa kamwe
hatutakubali kuona udharirishaji huo ukifanyika wa kufungisha vyeti vya bandia
kwenye hizo ndoa kwa sababu tu ya kutaka kujipatia umaarufu na vijihela”alisema
Hakuna maoni
Chapisha Maoni