Zinazobamba

WAZIRI MKUCHIKA AWATAKA WATENDAJI WA MKURABITA KUWAFUATA WAMACHINGA,SOMA HAPO KUJUA


Pichani ni Meneja Mratibu wa Mkurabita,Seraphia Robert akimkalibisha waziri Mkuchika 

WAZIRI wa nchi ,ofisi ya Rais -Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora,Kapteni George Mkuchika akizungumza na wafanyakazi wa Mkurabita pamoja na Waandishi wa habari alipofanya ziara ya kuongea na wafanyakazi wa Mkurabita
 NA KAROLI VINSENT 
WAZIRI wa nchi ,ofisi ya Rais -Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora,Kapteni George Mkuchika amewataka watendaji wa Mpango wa kurasimisha Rasilimali za Wanyonge (MKURABITA) kuhakikisha wanawasaidia wafanyabiashara wadogowadogo ili waweze kukopesheka.

Pia Waziri Mkuchika amewataka watendaji hao kutambua ofisi yao ipi chini ya Rais John Magufuli hivyo hawana Budi kufanya kazi kwa kuwatumikia wananchi kama ilivyo sera ya serikali ya awamu ya Tano.

Waziri Mkuchika ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa anafanya ziara ya kwenye Ofisi za  MKurabita ikiwa ni lengo ya kuangalia shughuli za utendaji.

Amesema ni wafanyabiashara wengi wadogo wamekuwa hawakuposheki kwenye taasisi za kifedha kutokana na kutokkuwa na dhamana.

"Hapa Dar kuna wamachinga wengi wanafanya Biashara hawana Mitaji ya kutokana na kukopesheka ,sasa ni wakati kwa Mkurabita  kushirikiana na serikali za mitaa kuangalia jinsi ya kuwasaidia wafanyabiashara hawa waweze kupata mikopo ili iweze kuwaisadia katika Biashara hizi"Amesema Waziri Mkuchika.

Hata Hivyo Waziri Mkuchika licha kuwapongeza watendaji wa Mkurabita amewataka kuhakikisha wanafanya kazi kwa moyo kwa kuwatumikia wananchi kwakuwa idara hiyo iko chini ya Rais.

"Serikali ya awamu ya Tano ni ya kuwatumikia wananchi,hivyo nawaomba mfanya kazi kwa bidii huku mkifahamu kuwa idara yenu ipo chini ya Rais ,hivyo hata kwenye kasi ya kufanya kazi iendane na kasi ya Rais "

Kwa upande wake Meneja Mratibu wa Mkurabita,Seraphia Robert amewambia Waziri Mkuchika kwa sasa wanachangomoto ya Rasilimali watu kutokana na kuwa na watendaji wachache katika kufanya kazi.
"Kwa sasa tuna idadi ndogo ya watumishi kutokana na kuwa na watumishi 23 tu  nchi nzima "amesema Bi Robert.

Amesema Licha ya kuwa na changamoto hiyo lakini wameweza kuwasaidia wananchi mbali mbali katika kujikwamua na hali ya umasikini.

Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge ulianzisha mwaka 2004 kwa lengo 
Wafanyakazi wa Ofisi ya Mkurabita wakiwa kwenye picha ya Pamoja na Waziri Mkuchika

Sehemu ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri Mkuchika