TECNO WAZINDUA SIMU PHANTOM 8 DUBAI
Dubai, United Arab Emirates, October 22, 2017 – TECNO, Kampuni kubwa ya simu
za mkononi TECNO iliyopo chini ya TRANSSION HOLDINGS , imetambulisha rasmi
simu yake mpya katika harakati zake za kukuza soko katika nchi za Asia na Africa, TECNO Phantom 8 katika jiji la Dubai.
Matumizi ya smartphone yanakua kwa kasi katika maeneo ya nchi za kiafrika na za mashariki ya kati kwa kiasi cha milioni 123. 7 mpaka 2016 toka milioni 106.4 mwaka 2015.
ushindani katika bara la Afrika na mashariki ya kati” Alisema makamu wa rais wa
kampuni
mama TRANSSION HOLDINGS, Arif Chowdhury. “Mipango yetu ni mwaka jana ilikua
kukua zaidi kupitia mashariki ya kati hivyo kuzindua rasmi Phantom 8 jiijini Dubai
ni hatua mojawapo
katika kuendeleza mipango hii. Simu zetu zitaendelea kujikita katika kufuata mahitaji ya
wateja zaidi”. Alimaliza Makamu wa raisi.
TECNO Mobile inaendelea kutoa bidhaa zenye ubora kwa wateja wake hasa barani
Africa ambapo kampuni hiyo ina nafasi kubwa katika mauzo hasa kwa nchi kama
Tanzania na Nigeria na nchi kadhaa kutokea mashariki ya kati.
Kwa zaidi ya miaka 11 TECNO imekua ikifanya kazi ya kuunganisha wananchi katika mawasiliano kupitia simu hasa kwa kuleta simu zenye ubora na bei inayoendana
na watumiaji wake.
Simu hiyo iliyozinduliwa jijini Dubai imekua gumzo tangu tetesi zitoke kua inakuja sokoni imezinduliwa ikiwa na jina la Phantom 8 huku ikiwa imetengenezwa kwa teknolojia kubwa hasa kwa upande wa kamera ikiwa na megapixel 20 mbele na kamera mbili
nyuma6 GB RAM na ROM ikiwa ni 64GB. Kwa upande wa dizaini simu
inametengenezwa vizuri ikiwa na muundo wa mithili ya Almasi na kioo.
Phantom 8 kutarajiwa kufika mabara mengine pia duniani.
Phantom 8 inauwezo wa kuweka “simcard” aina ya “Nano/ Micro” na inauwezo wa kumud memory card ya hadi 2TB (Terra Bytes) na pia inauwezo wa 4G plus
ambayo inakuwezesha kutumia simu yako ndani na Zaidi ya nchi 200.
Kwa wateja waliopo Tanzania wataweza kuagiza simu hii mpya katika maduka maalumu ya simu za TECNO ili kuweza kuipata inapoingia sokoni siku chache zijazo.
Phantom 8 iliyozinduliwa hivi karibuni iikiwa imesheheni na sifa za kipekee kama Kamera, Ubo na muonekano wa kipekee pamoja na kasi ya ajabu. Kamera ikiw ana uwezo wa 20 MP,
pamoja na kamera pacha zenye uwezo wa 13Mp +12 Mp kamera za nyuma ikiambatana na uwezo wa kuvuta picha mara 10 zaidi ya kamera ya kawaida, Ina uwezo wa HDR,
4 in 1 uwezo wa kungarisha picha,AF na mambo mengine mengi yenye kukuhahkishia
kupata picha zilizo bora na zenye muonekano mzuri.
Kwa maelezo zaidi kuhusian na TECNO Mobile tembelea https://www.tecno-mobile.com/index.php?m=Home&c=Index&a=index
###